Loading...
title : NEWS ALERT: CGP KASIKE AFANYA MABADAILIKO MAKUBWA WAKUU WA MAGEREZA MIKOA TANZANIA BARA
link : NEWS ALERT: CGP KASIKE AFANYA MABADAILIKO MAKUBWA WAKUU WA MAGEREZA MIKOA TANZANIA BARA
NEWS ALERT: CGP KASIKE AFANYA MABADAILIKO MAKUBWA WAKUU WA MAGEREZA MIKOA TANZANIA BARA
Katika kuboresha utendaji kazi ndani ya Jeshi la Magereza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Martin Kasike amefanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi kwa kuwateua Wakuu wa Magereza wa Mikoa Tanzania Bara(RPOs) 19 wapya na saba (7) kuwabakiza katika nyadhifa zao.
Katika mabadiliko hayo Kamishna Jenerali Kasike ameteuwa na kuthibitisha maafisa sita (6) kuwa Wakuu wa Vyuo vya Magereza na kuwabadilisha maafisa wengine watatu (3) katika vitengo muhimu ndani ya Jeshi hilo.
Aidha, Kamishna Jenerali Kasike katika mabadiliko hayo kwa mara ya kwanza amewateua Wakuu wa Magereza wa Mikoa katika mikoa ya Katavi, Songwe, Njombe, Simiyu na Geita ambayo ilikuwa haina uongozi wa kimagereza katika ngazi ya mikoa hiyo.
Katika mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa RPO (DSM) SACP. Hamis Nkubasi ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza kitengo cha Ujenzi na nafasi yake kuchukuliwa na SACP. Julius Ntambala, SACP. Salum Hussein RPO (Dodoma) amebakia katika kituo chake na aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kiwira SACP. Luhende Makwaia anakwenda kuwa RPO (Mbeya) na nafasi yake kuchukuliwa na ACP. Mathias Mkama na aliyekuwa RPO (Mbeya) SACP. Kijida Mwakingi amehamishiwa Makao Makuu, Kitengo cha TEHAMA.
Aliyekuwa RPO (Mtwara) SACP. Ismail Mlawa amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza Kitengo cha Mipango na nafasi yake kuchukuliwa na ACP. Varisanga Msuya aliyekuwa Kaimu Bohari Mkuu wa Jeshi ambapo nafasi yake inachukuliwa na ACP. Robert Masali ambaye anakuwa Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza. Aliyekuwa RPO (Mwanza) SACP. Athuman Kitiku amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza sehemu ya Utumishi na nafasi yake kuchukuliwa na SACP. Hamza Hamza aliyekuwa RPO Tabora.
Aidha, ACP. Joseph Mkude anakuwa RPO (Tabora) na aliyekuwa RPO (Kagera) SACP. Boyd Mwambingu amehamishiwa Makao Makuu Kitengo cha Utawala na nafasi yake inachukuliwa na ACP. Rymond Mwampashe. Aliyekuwa RPO (Lindi) SACP. Rajabu Bakari amehamishiwa Makao Makuu Kitengo cha Mawasiliano na Usafirishaji na nafasi yake kuchukuliwa na ACP. Josephine Semwenda.
Aliyekuwa RPO (Rukwa) SACP. Benno Hunja amehamishiwa Makao Makuu sehemu ya Kilimo, Mifugo na Mazingira na nafasi yake inachukuliwa na ACP. Jail Mwamgunda na aliyekuwa RPO (Kilimanjaro) SACP. Hassan Mkwiche amehamishiwa Makao Makuu kuwa Mkuu wa Kitengo cha Afya, Tiba na Lishe na nafasi yake kuchukuliwa na ACP. Rajab Igongi. Aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Afya, Tiba na Lishe ACP. Wilson Rugamba anakuwa RPO (Shinyanga).
Hivyo makala NEWS ALERT: CGP KASIKE AFANYA MABADAILIKO MAKUBWA WAKUU WA MAGEREZA MIKOA TANZANIA BARA
yaani makala yote NEWS ALERT: CGP KASIKE AFANYA MABADAILIKO MAKUBWA WAKUU WA MAGEREZA MIKOA TANZANIA BARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NEWS ALERT: CGP KASIKE AFANYA MABADAILIKO MAKUBWA WAKUU WA MAGEREZA MIKOA TANZANIA BARA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/news-alert-cgp-kasike-afanya.html
0 Response to "NEWS ALERT: CGP KASIKE AFANYA MABADAILIKO MAKUBWA WAKUU WA MAGEREZA MIKOA TANZANIA BARA"
Post a Comment