Loading...
title : UJUMBE MKUBWA WA SEKTA BINAFASI ZA MAFUTA NCHINI UGANDA WAONYESHA NIA YA KUPITISHA BIDHAA BANDARI YA TANGA
link : UJUMBE MKUBWA WA SEKTA BINAFASI ZA MAFUTA NCHINI UGANDA WAONYESHA NIA YA KUPITISHA BIDHAA BANDARI YA TANGA
UJUMBE MKUBWA WA SEKTA BINAFASI ZA MAFUTA NCHINI UGANDA WAONYESHA NIA YA KUPITISHA BIDHAA BANDARI YA TANGA
UJUMBE Mkubwa wa Sekta Binafsi za mafuta na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kutoka nchini Uganda leo wametembelea Bandari ya Tanga huku wakionyesha nia yao ya kutumia Bandari ya Tanga kupitisha bidhaa zao kutokana na uwezo wa kupunguza gharama kwa zaidi ya asilimia 30 mpaka 45 ikiwemo kutumia muda mfupi kuhudumia shehena.
Hayo yalisemwa na Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama mara baada ya ujumbe huo kutembelea Bandari ya Tanga ikiwemo maeneo yatakapojengwa matenki makubwa ya mafuta ghafi yatakayotoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga eneo la Chongoleani.
Alisema kwamba lengo la ujumbe huo kutua mkoani Tanga ni kuangalia fursa eneo gani ambalo wanaweza kupitisha bidhaa zao kutoka nchini Uganda kwenda kwenye soko la nje kwa gharama nafuu zaidi na kupelekwa pia eneo ambalo litapokelea mafuta, Bohari ya Mafuta Mkoani Tanga ya GBP na sehemu ambayo mafuta yanaposhushwa (Gati ya Meli za mafuta).
“Kwa kweli tunawashukuru TPA makao makuu na Serikali kutuletea ujumbe huu mkubwa wa sekta binafsi za mafuta za Uganda wakiwemo Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano ya Uganda jambo ambalo linatusaidia kutangaza fursa kubwa tulionayo Bandari yetu ya Tanga “Alisema.
Alisema msingi wake wa kutumia muda mfupi wakati wa upitishaji wa bidhaa msingi wake ni meli kwenye Bandari ya Tanga inakuja moja kwa moja inapata gati tofauti na maeneo mengine unalazimika kusubiri kwa kipindi cha wiki moja mpaka mbili ambapo kitaalamu wanasema dunia kwenye biashara za bandari na meli katika kila sh, mia moja mwenye meli anaingia gharama ya s h.65 akiwa bandarini.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akizungumza na UJUMBE Mkubwa wa Sekta Binafsi za mafuta na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kutoka nchini Uganda waliotembelea Bandari ya Tanga na maeneo mengine
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akisalimiana na UJUMBE Mkubwa wa Sekta Binafsi za mafuta na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kutoka nchini Uganda waliotembelea ofisini kwake kabla ya kutembelea Bandari ya Tanga na maeneo mengine
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama katika akiwa na baadhi ya wajumbe wakiwa eneo la yatakapojengwa matenki makubwa ya mafuta ghafi yatakayotoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga eneo la Chongoleani.
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto akitoa maelezo kwa wajumbe hao wakati wakiwa eneo la yatakapojengwa matenki makubwa ya mafuta ghafi yatakayotoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga eneo la Chongoleani. HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>> |
Hivyo makala UJUMBE MKUBWA WA SEKTA BINAFASI ZA MAFUTA NCHINI UGANDA WAONYESHA NIA YA KUPITISHA BIDHAA BANDARI YA TANGA
yaani makala yote UJUMBE MKUBWA WA SEKTA BINAFASI ZA MAFUTA NCHINI UGANDA WAONYESHA NIA YA KUPITISHA BIDHAA BANDARI YA TANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UJUMBE MKUBWA WA SEKTA BINAFASI ZA MAFUTA NCHINI UGANDA WAONYESHA NIA YA KUPITISHA BIDHAA BANDARI YA TANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/ujumbe-mkubwa-wa-sekta-binafasi-za.html
0 Response to "UJUMBE MKUBWA WA SEKTA BINAFASI ZA MAFUTA NCHINI UGANDA WAONYESHA NIA YA KUPITISHA BIDHAA BANDARI YA TANGA"
Post a Comment