Loading...
title : WAZIRI DKT.KIGWANGALLA AWATUNUKU VYETI WAHITIMU 289 WA CHUO CHA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI-MWEKA
link : WAZIRI DKT.KIGWANGALLA AWATUNUKU VYETI WAHITIMU 289 WA CHUO CHA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI-MWEKA
WAZIRI DKT.KIGWANGALLA AWATUNUKU VYETI WAHITIMU 289 WA CHUO CHA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI-MWEKA
Na Andrew Chale,Moshi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla amewataka watumishi walio kwenye Wizara yake hiyo kupitia mafunzo ya Jeshi Usu ili kujiimalisha zaidi katika kutokomeza vitendo vya ujangili wa Maliasili zilizopo sehemu mbalimbali hapa nchini.
Waziri Dkt. Kigwangalla amesema hayo Novemba 24, 2018 wakati wa kuwatunuku vyeti wahitimu 289 katika kozi mbalimbali ikiwemo Shahada, Stashahada na Astashada kwenye Usimamizi wa Wanyamapori na Utalii kwenye Mahafali ya 54 ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori- Mweka, Wilayani Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Akielezea suala la kupata mafunzo kwa watumishi hao, amesema suala hilo la uhifadhi ni la kudumu hivyo ni vyema watumishi hao kujiandaa katika ulinzi wa Maliasili za Taifa.Dkt Kigwangalla amesema mifumo wanayotengeneza ikiwemo Jeshi Usu lazima ifanye kazi imara na iwe madhubuti ili kusaidia kulinda Malisili zilizopo kwani hali ya uvamizi wa wananchi na waalifu wa Maliasili za taifa ni kubwa.
“Kama Serikali tuna nia na dhamira ya dhati ya kulinda na uhifadhi Maliasili tulizonazo ambazo ni urithi sio tu kwa watoto wetu hapa Tanzania, lakini ni urithi wa vizazi na vizazi vya Dunia yote” amesema Dkt. Kigwangalla.Aidha, Waziri Dkt. Kigwangalla ametoa wiki mbili kuanzia Novemba 24, kwa taasisi nne zilizo chini ya Wizara hiyo Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa kila kutoa Shilingi Milioni 100 ilikuchangia ujenzi wa jengo la Utawala na mafunzo chuoni hapo ili kuanza mara moja ujenzi wa jengo hilo jipya.
Waziri wa Maliasi na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akimtunuku cheti Mhitimu wa Shahada ya Usimamizi wa Wanyamapori, katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka katika mahafali ya 54 yaliyofanyika jana Novemba 24, 2018 chuoni hapo katika wilaya ya Moshi mkoani Kiliamanjaro. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Jafari Kideghesho. Jumla ya wahitimu 289, wa kozi mbalimbali walitunukiwa vyeti.
Waziri akicheza muziki wa Kwaito na wahitimu
Waziri akizungumza katika mahafali hayo

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi na Maliasili Nape Nnauye akizungumza katika tukio hilo.
Waziri wa Maliasi na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akipokea zawadi ya picha ya kuchorwa aliyochorwa na mwanafunzi wa chuo hicho (kushoto) anayemkabidhi. Wakati wa tukio la kukabidhi zawadi katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka katika mahafali ya 54 yaliyofanyika jana Novemba 24, 2018 chuoni hapo katika wilaya ya Moshi mkoani Kiliamanjaro.

Hivyo makala WAZIRI DKT.KIGWANGALLA AWATUNUKU VYETI WAHITIMU 289 WA CHUO CHA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI-MWEKA
yaani makala yote WAZIRI DKT.KIGWANGALLA AWATUNUKU VYETI WAHITIMU 289 WA CHUO CHA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI-MWEKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI DKT.KIGWANGALLA AWATUNUKU VYETI WAHITIMU 289 WA CHUO CHA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI-MWEKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/waziri-dktkigwangalla-awatunuku-vyeti.html
0 Response to "WAZIRI DKT.KIGWANGALLA AWATUNUKU VYETI WAHITIMU 289 WA CHUO CHA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI-MWEKA"
Post a Comment