Loading...
title : FAIDA YA MAADHIMISHO NA MWENYEZI MUNGU
link : FAIDA YA MAADHIMISHO NA MWENYEZI MUNGU
FAIDA YA MAADHIMISHO NA MWENYEZI MUNGU

Askofu mkuu wa Tanzania Assemblies of God (TAG) Dkt. Barnabas Mtokambali amesema Mwenyezi Mungu anapenda maadhimisho kwa kuwa ni sehemu ya kujifunza, kumsifu, kujenga ushirika na kumtolea shukran. Dkt. Mtokambali amebainisha hayo Mjini Dodoma, kwenye sherehe za maadhimisho ya mchungaji Vangast Salum wa kanisa la TAG, kwa kutimiza miaka 40 ya wokovu na 36 ya huduma na kuweka wakfu kitabu.
Amesema moja ya sababu za maadhimisho ni kujifunza, akitolea mfano mchungaji Vangast Salum, amepitia hatua mbalimbali za maisha na kiuchungaji na kwamba maadhimisho pia yanajenga ushirika zaidi na Mwenyezi Mungu kwa kuwaleta watu karibu.
Kiongozi huyo wa juu wa kanisa la TAG Tanzania amesema kuwa sababu ya tatu ya maadhimisho ni kumsifu Mwenyezi Mungu kwa yote aliyoyafanya juu ya maisha ya mchungaji Vangast Salum kwa kipindi cha miaka 40 ya wokovu, na kumtaka kutoa shukran za kumsifu Mwenyezi Mungu.
Wakati huo huo Askofu mkuu wa Tanzania Assemblies of God (TAG) Dkt. Barnabas Mtokambali amepata fursa ya kuzindua vitabu 500 vya mafundisho ya dini na uzinduzi wa jengo la darasa na Ofisi ya mchungaji wa kanisa hilo eneo la Area D Mjini Dodoma.
Hivyo makala FAIDA YA MAADHIMISHO NA MWENYEZI MUNGU
yaani makala yote FAIDA YA MAADHIMISHO NA MWENYEZI MUNGU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala FAIDA YA MAADHIMISHO NA MWENYEZI MUNGU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/faida-ya-maadhimisho-na-mwenyezi-mungu.html
0 Response to "FAIDA YA MAADHIMISHO NA MWENYEZI MUNGU"
Post a Comment