Loading...

Shule tatu Kibamba zakabidhiwa visima

Loading...
Shule tatu Kibamba zakabidhiwa visima - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Shule tatu Kibamba zakabidhiwa visima, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Shule tatu Kibamba zakabidhiwa visima
link : Shule tatu Kibamba zakabidhiwa visima

soma pia


Shule tatu Kibamba zakabidhiwa visima

Joseph Zablon

Shirika lisilo la kiserikali la Time to Help limekabidhi visima vitatu kwa shule tofauti za wilaya mpya ya Kibamba, jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mpango wa taasisi hiyo kusaidia shule za msingi na sekondari nchini katika kukabili changamoto tofauti.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa shule za sekondari Kibwegere, Kibweheri na shule za msingi Kibwegere, leo Mkuu wa tasisi hiyo Kubilaty Talu alisema wametoa msaada huo baada ya kuombwa kufanya hivyo.

Alisema tasisi hiyo imelenga kuzisaidia shule mbalimbali nchini kukabili changamoto ya mahitaji ya maji na visima hivyo anaamini vitabadili mazingira na kuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wa shule hizo tatu ambao pia walipewa zawadi za madaftari.awali Naibu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibwegere, Halima Mgaya alisema visima hivyo vitasaidia mengi ikiwa ni pamoja na kulinda afya za watoto kutokana na uhaba wa maji hivyo pia kuwaepusha na magonjwa yanayotokana na uhaba wa maji safi na salama.

Katika risala ya wanafunzi wa sule hiyo hizo ambayo iliwasilishwa kwa mtindo wa ngonjera, wanafunzi wa shule hizo waliomba msaada wa vyumba zaidi vya madarasa kutokana na uhaba uliopo na wameshukuru kupata huduma ya maji.Walisema ukosefu wa maji safi na salama ulisababisha baadhi ya wanafunzi kuugua magonjwa ya matumbo mara kwa mara kutokana na kutumia maji ya kunywa yasiyo safi wala salama. 
Mlezi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Time to help, Remziye Talu akifungua bomba la maji jana, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima cha maji katika shule ya sekondari Kibwegere ambacho kimejengwa na taasisi hiyo, Kibamba, Dar es Salaam.
Mlezi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Time to help, Remziye Talu akifungua bomba la maji jana, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima cha maji katika shule ya sekondari Kibwegere ambacho kimejengwa na taasisi hiyo, Kibamba, Dar es Salaam.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Kibwegere (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibweheri, Alexandra Ngonyani na Naibu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibwegere, Halima Mgaya, wakimshukuru mlezi wa taasisi ya Time to help, Remziye Talu (kulia) mara baada ya uzinduzi wa kisima kilichojengwa na taasisi hiyo katika shule ya sekondari Kibwegere
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kibwegere wakipewa madaftari na zawadi zingine kutoka kwa wahisani wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Time to help mara baada ya uzinduzi wa kisima cha maji katika Shule ya Sekondari Kibwegere, jana. Taasisi hiyo imekabidhi visima vya maji vitatu katika shule za sekondari Kibweheri , Kibwegere shule ya msingi Kibwegere.



Hivyo makala Shule tatu Kibamba zakabidhiwa visima

yaani makala yote Shule tatu Kibamba zakabidhiwa visima Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Shule tatu Kibamba zakabidhiwa visima mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/shule-tatu-kibamba-zakabidhiwa-visima.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Shule tatu Kibamba zakabidhiwa visima"

Post a Comment

Loading...