Loading...
title : Fast Jet kufilisika?
link : Fast Jet kufilisika?
Fast Jet kufilisika?
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesema Shirika la Ndege la Fastjet limepoteza sifa ya kufanya biashara nchini, hivyo limezuia ndege moja ya shirika hilo kuruka kutokana na matatizo ya mara kwa mara na kukosekana kwa meneja mwajibikaji wa shirika.
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, Hamza Johari leo Jumatatu Desemba 17, 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Amesema tayari TCAA imetoa notisi ya siku 28 kuanzia leo ya kusudio la kufuta leseni ya shirika hilo.
"Tumekuwa tukiwaandikia barua ya kuwataka watueleze kuhusu mwenendo wao wa biashara tangu Fastjet Plc wajiondoe lakini pia shirika limekuwa na madeni mbalimbali ambayo hayajalipwa. Tukiomba watupe mpango wao wa fedha na biashara kwa mujibu wa sheria hawafanyi hivyo," amesema Johari.
Amesema shirika hilo linadaiwa na watoa huduma wake wengi ikiwemo TCAA inayolidai Sh1.4 bilioni lakini pia halina meneja mwajibikaji ambaye ni mtaalamu wa masuala ya ndege anayepaswa kutoa majibu ya hali ya ndege.
"Kwa sasa fastjet hawana ndege. Ndege yao tangu jana tumeizuia kuruka kwa kuwa imekuwa ikipata hitilafu mara kwa mara na hawana mtu ambaye anaweza kutoa taarifa kuhusu mwenendo wake jambo ambalo linahatarisha usalama endapo itaruka," amesema Johari.

Hivyo makala Fast Jet kufilisika?
yaani makala yote Fast Jet kufilisika? Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Fast Jet kufilisika? mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/fast-jet-kufilisika.html
0 Response to "Fast Jet kufilisika?"
Post a Comment