Loading...

HIKI NDICHO WATOTO YATIMA WANAHITAJI KIPINDI CHA SIKUKUU

Loading...
HIKI NDICHO WATOTO YATIMA WANAHITAJI KIPINDI CHA SIKUKUU - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa HIKI NDICHO WATOTO YATIMA WANAHITAJI KIPINDI CHA SIKUKUU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : HIKI NDICHO WATOTO YATIMA WANAHITAJI KIPINDI CHA SIKUKUU
link : HIKI NDICHO WATOTO YATIMA WANAHITAJI KIPINDI CHA SIKUKUU

soma pia


HIKI NDICHO WATOTO YATIMA WANAHITAJI KIPINDI CHA SIKUKUU


IMEKUWA kawaida kwa jamii ya kitanzania kushiriki na watoto wanaolelewa katika vituo vya watoto wenye uhitaji chakula na mahitaji mengine hususan katika msimu wa Sikukuu

Mwananchi mmoja mmoja , vikundi taasisi na ofisi mbalimbali za Serikali na binafsi zimekuwa zikitoa msaada wa chakula na mahitaji mengine kwa vituo vya watu wenye uhitaji lakini je umeshawahi jiuliza watoto hao wanahitaji nini zaidi?

“Mimi napenda sana mtu akipeleke kuogelea lakini, Sisi tunataka kutoka na kujumuika na  watu wengine tucheze nao na tufurahi badala ya wao kuja kutuachia chakula tuu nakuondoka “ alisema Mudy Mbeki mtoto anayelelewa katika kituo cha Yatima Group Trust Fund Chamazi ambaye alikuwa akisherehekea Sikukuu ya Krismass ikiwa ni maadhimisho ya Wakristo ulimwenguni kote  wakikumbuka kuzaliwa kwa masihi Yesu Kristu.

Mudy ni mmoja kati ya watoto zaidi ya 250 kutoka vituo viwili vya watoto wenye uhitaji vya Yatima Group Trust Fund Chamazi na Kurasini Orphanage Center waliokutanishwa pamoja katika ukumbi wa kifarahi katika hoteli ya The Dar es salaam serena Hotel kusherehekea na wafanyakazi pamoja na wadau wa serena msimu huu wa sikukuu.

“Tumekodi zaidi ya magari matano  kwenda kuwafata watoto katika vituo vyak Kurasini na Chamanzi ili wawalete watoto hapa Serena Hotel tufurahi nao sikukuu hii, na huu ni utamaduni wetu wa miaka mingi baada ya kugundua watoto wanatakq sana kutoka nje ya makazi yao waliozoea kipindi hiki cha sikukuu” alisema Sophia Mketo Meneja Rasilimali watu wa Hoteli ya Serena.  

Aliongeza kuwa sherehe hiyo wameshirikiana na wadau wa serena kwa kuwanunulia zawadi watoto wote waliofika hapo kwenye sherehe na lengo kuu ni kuhakikisha watoto wanakuwa na furaha na kuona wanathaminiwa. 

Amesema hapo awali walikuwa wakipika chakula na kupeleka vituoni lakini watoto hao ndio walioonesha hamu ya kutaka kutoka nje ya vituo ndipo walipoanza utamaduni wa kuwatoa outing na imeendelea hivyo kwa miaka mitatu mfululizo sasa. 
 Watoto Yatima wakiwa pamoja na baadhi ya viongozi wao walipokuwa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
Mwandishi na Mtangazaji maarufu Leaa Mushi (aliyebeba mtoto huku akiwa amebeba mkoba)akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto yatima waliokuwa na viongozi wao wakifurahia msimu huu wa Sikukuu.



Hivyo makala HIKI NDICHO WATOTO YATIMA WANAHITAJI KIPINDI CHA SIKUKUU

yaani makala yote HIKI NDICHO WATOTO YATIMA WANAHITAJI KIPINDI CHA SIKUKUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala HIKI NDICHO WATOTO YATIMA WANAHITAJI KIPINDI CHA SIKUKUU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/hiki-ndicho-watoto-yatima-wanahitaji.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "HIKI NDICHO WATOTO YATIMA WANAHITAJI KIPINDI CHA SIKUKUU"

Post a Comment

Loading...