Loading...
title : UDHIBITI UCHAKUAJI MAFUTA WAVUTIA WAWEKEZAJI UINGEREZA
link : UDHIBITI UCHAKUAJI MAFUTA WAVUTIA WAWEKEZAJI UINGEREZA
UDHIBITI UCHAKUAJI MAFUTA WAVUTIA WAWEKEZAJI UINGEREZA
Na Seif Mangwangi ,Arusha
FURSA na mazingira mazuri ya biashara ya uuzaji mafuta nchini yametajwa kuanza kuvutia wawekezaji ambapo Kampuni ya Vivo Energy Plc ya Uingereza imepanga kuwekeza mtaji wa dola Milioni3 kwa mwaka ifikapo Machi mwakani.
Akizungumza jana mkoani hapa Mkurugenzi Mtendaji wa Engen Petroleum (Tanzania Ltd), Paul Muhato alisema, mazingira mazuri yameishawishi Vivo Energy Plc kujuna nchini na kuwekeza Dola za Marekani milioni 3 kila mwaka.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha kuuzia mafuta cha Engen kilichopo Tengeru wilayani Arumeru Muhato alisema, kumekuwa na udhibiti mkubwa wa njia za panya zilizokuwa zikiingiza mafuta nchini.
“Udhibiti huu umesaidia sana kuziba njia za panya ambapo mafuta mengi yaliingia nchini bila kulipiwa kodi na hivyo kusababisha kusiwepo uwiano wa kibiashara,” alisema Muhato na kuongeza:“Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), na Taasisi nyingine za Serikali kuweka kodi sawa kwa mafuta ya taa na dizeli,” alisema.
Alisema licha ya kodi kuwa sawa, baadhi ya kampuni zilikosa uaminifu na kuingiza mafuta ya taa kutoka Kenya kutokana na kodi ya mafuta hayo ilikuwa chini ikilinganishwa na Tanzania.Aidha kutokana na nchi ya Kenya kurekebisha kodi kwa mafuta ya dizeli na taa iliwezesha kuweka mizania sawa na hivyo Kampuni zilizoingiza mafuta kwa lengo la kuchakachua hazikuweza tena.
.Mkurugenzi Mtendaji wa Engen Petroleum Paul Muhato wa sita kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja mbele ya kituo kipya cha mafuta cha engen alichokizindua jana jijini Arusha
Mkurugenzi mtendaji wa Engen Petroleum ltd Paul Muhato akikata utepe kuashiria kuzindua kituo kipya cha mafuta cha Engen Tengeru Arusha jana.
Mkazi wa Tengeru akihudumiwa mafuta katika kituo kipya cha mafuta cha Engen kilichozinduliwa jana
Hivyo makala UDHIBITI UCHAKUAJI MAFUTA WAVUTIA WAWEKEZAJI UINGEREZA
yaani makala yote UDHIBITI UCHAKUAJI MAFUTA WAVUTIA WAWEKEZAJI UINGEREZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UDHIBITI UCHAKUAJI MAFUTA WAVUTIA WAWEKEZAJI UINGEREZA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/udhibiti-uchakuaji-mafuta-wavutia.html
0 Response to "UDHIBITI UCHAKUAJI MAFUTA WAVUTIA WAWEKEZAJI UINGEREZA"
Post a Comment