Loading...
title : MAKONDA ATOA AGIZO KUCHUNGUZA WANADAIWA KUUZA VITAMBULISHO VYA UJASILIAMALI, AKIGAWA NG'OMBE WA SIKUKUU.
link : MAKONDA ATOA AGIZO KUCHUNGUZA WANADAIWA KUUZA VITAMBULISHO VYA UJASILIAMALI, AKIGAWA NG'OMBE WA SIKUKUU.
MAKONDA ATOA AGIZO KUCHUNGUZA WANADAIWA KUUZA VITAMBULISHO VYA UJASILIAMALI, AKIGAWA NG'OMBE WA SIKUKUU.
Na. John Luhende
Mwamba wahabari
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ,amemwagiza Kamanda wa kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamishina wa Polisi Lazaro Mambo sasa kuunda timu ya uchunguzi kubaini watu wanaodaiwa kuuza vitambulisho vya ujasiliamali vilivyo tolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Makonda ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza katika zoezi la kugawa ng’ombe wa sikukuu kwa Jeshi la wananchi wa Tanzania ,Jeshi la polisi na watumishi wa Afya katika hospitali za koa wa Dar es salaam na kuagiza kukamatwa kwa watakao bainika kujihusisha na vitendo hivyo.
Aidha Makonda ameelezwa kutoridhishwa na zoezi la kugawa vitambulisho vya ujasilia mali katika Wilya za Temeke, Ubungo, Kinondoni na Ilala, nakuagiza ifikapo January 6 liwe limekamilika.
Kwa upande wake Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamishina Lazaro Mambo sasa akizungumza katika zoezi hilo amemshukuru RC Makonda na kuahidi kudumisha ulinzi wakati wa sikuu ya Mwaka mpya.
Pamoja na hayo RC Makonda amelipongeza Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ na Jeshi la Polisi kuendelea kudumisha amani nakushiriki katika kazi na huduma mbalimbali za kijamii mkoani humo.
"Leo nawapatia Polisi Ng'ombe 20, Jeshi la Wananchi ng'ombe 20, na wafanyakazi wa Hospitali ya Mwananyamala, Temeke na Amana nao nawapatia ng'ombe 20,watakula na wagonjwa wao waliopo wodini siku ya mwaka mpya" alisema.
Amewashukuru pia wadau waliwezesha kupatikana kana kwa ng'ombe hao akiwemo Naibu Meya wa Maispaa ya Ilala ambaye pia ni diwani wa kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto.
"Huyo Diwani wenu ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, nilimwambia nayeye Anitafutie Ng'ombe na ameleta asinge leta inamaana as ingekuwa na sifa ya kuwa kiongozi wa eneo hili" Alisema
Hivyo makala MAKONDA ATOA AGIZO KUCHUNGUZA WANADAIWA KUUZA VITAMBULISHO VYA UJASILIAMALI, AKIGAWA NG'OMBE WA SIKUKUU.
yaani makala yote MAKONDA ATOA AGIZO KUCHUNGUZA WANADAIWA KUUZA VITAMBULISHO VYA UJASILIAMALI, AKIGAWA NG'OMBE WA SIKUKUU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKONDA ATOA AGIZO KUCHUNGUZA WANADAIWA KUUZA VITAMBULISHO VYA UJASILIAMALI, AKIGAWA NG'OMBE WA SIKUKUU. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/makonda-atoa-agizo-kuchunguza-wanadaiwa.html
0 Response to "MAKONDA ATOA AGIZO KUCHUNGUZA WANADAIWA KUUZA VITAMBULISHO VYA UJASILIAMALI, AKIGAWA NG'OMBE WA SIKUKUU."
Post a Comment