Loading...
title : Naibu Waziri wa Nishati aendelea kuwasha umeme vijijini mkoani Ruvuma
link : Naibu Waziri wa Nishati aendelea kuwasha umeme vijijini mkoani Ruvuma
Naibu Waziri wa Nishati aendelea kuwasha umeme vijijini mkoani Ruvuma
Na Teresia Mhagama, Ruvuma
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, ameendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi ya umeme mkoani Ruvuma ambapo leo amewasha umeme Kijiji cha Palangu na Mang’ua pamoja mtaa wa Luhila Seko katika Wilaya ya Songea ambavyo vimepata umeme kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) mzunguko wa kwanza na mradi wa Makambako – Songea.
Huo ni muendelezo wa kazi ya ukaguzi na uzinduzi wa miradi ya umeme vijijini mkoani Ruvuma aliyoianza tarehe 17 Disemba, 2018 kwa kuwasha umeme katika Vijiji Saba vilivyopo katika Wilaya ya Tunduru na Namtumbo ambapo wateja zaidi ya 200 wameunganishwa na huduma ya umeme.
Aidha, kuunganishwa kwa umeme katika Vijiji Palangu, Mang’ua pamoja na Mtaa wa Luhila Seko, wilayani Songea kumewezesha wateja zaidi ya 230 kuunganishwa na huduma hiyo huku wengine wakitumia umeme huo kwa shughuli za kiuchumi kama kusaga na kukoboa nafaka.
Pamoja na kuwasha umeme katika Vijiji hivyo, Naibu Waziri alikagua kazi ya usambazaji umeme katika Vijiji vya Liula, Mpangula na Litapwasi na kumsisitiza mkandarasi, kampuni ya Namis kufanya kazi kwa kasi na umakini ili kuondoa malalamiko ya wananchi ya kucheleweshewa huduma ya umeme.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasha rasmi umeme katika Kijiji cha Palangu wilayani Songea, mkoani Ruvuma. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololiti Mgema.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ( wa pili kulia) akiwasha rasmi umeme katika Kijiji cha Mang’ua wilayani Songea, mkoani Ruvuma. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololiti Mgema.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa tatu kulia) akiangalia kazi ya ukoboaji na usagaji wa nafaka katika Kijiji cha Mang’ua wilayani Songea, mkoani Ruvuma baada ya kijiji hicho kupata umeme. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololiti Mgema.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kulia) akikagua mitambo ya umeme katika kituo cha kupoza umeme cha Songea ambacho kimejengwa kupitia mradi wa umeme wa Makambako-Songea na kimeanza kusambaza umeme wa gridi kuanzia mwezi wa Tisa mwaka huu.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Naibu Waziri wa Nishati aendelea kuwasha umeme vijijini mkoani Ruvuma
yaani makala yote Naibu Waziri wa Nishati aendelea kuwasha umeme vijijini mkoani Ruvuma Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Waziri wa Nishati aendelea kuwasha umeme vijijini mkoani Ruvuma mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/naibu-waziri-wa-nishati-aendelea.html
0 Response to "Naibu Waziri wa Nishati aendelea kuwasha umeme vijijini mkoani Ruvuma"
Post a Comment