Loading...
title : Watanzania waaswa kuwa wamoja
link : Watanzania waaswa kuwa wamoja
Watanzania waaswa kuwa wamoja
Watanzania wametakiwa kuwa wamoja na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kwa kumuombea dua katika kipindi hiki ambacho nchi inapitia kipindi cha mabadiliko makubwa ya kiuchumi huku Serikali ikikataa kupokea misaada yenye masharti ya kudhalilisha mila na desturi za Watanzania.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati akimuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika Dua Maalumu ya Kumuombea Rais Magufuli na Kuombea Amani Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa, iliyoandaliwa na Taasisi ya Kidini ya Maridhiano Tanzania, katika Ukumbi wa Mikutano wa Sabasaba,jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa maombi hayo Naibu Waziri Masauni alisema nchi sasa inapitia kipindi cha mabadiliko makubwa ya kiuchumi yanayosimamiwa na Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli lengo ikiwa ni kuifanya Tanzania isiwe tegemezi na kupewa masharti yanayodhalilisha mila, tamaduni na dini zetu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa Dua Maalumu ya Kumuombea Rais kwa kutimiza Miaka mitatu madarakani na Kuombea Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa.Kulia ni Askofu Silvestre Gamanywa na Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania iliyoandaa maombi hayo, Asha Kassim.Maombi hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Sabasaba, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Sheikh Nurdin Mangochi akizungumza wakati wa Dua Maalumu ya Kumuombea Rais kwa kutimiza Miaka mitatu madarakani na Kuombea Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa..Maombi hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
Askofu Silvestre Gamanywa akizungumza wakati wa Dua Maalumu ya Kumuombea Rais kwa kutimiza Miaka mitatu madarakani na Kuombea Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa.Maombi hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa dini wakiwa katika Dua Maalumu ya Kumuombea Rais kwa kutimiza Miaka mitatu madarakani na Kuombea Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa. Maombi hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Sabasaba, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Watanzania waaswa kuwa wamoja
yaani makala yote Watanzania waaswa kuwa wamoja Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Watanzania waaswa kuwa wamoja mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/watanzania-waaswa-kuwa-wamoja.html
0 Response to "Watanzania waaswa kuwa wamoja"
Post a Comment