Loading...
title : SALAMU ZA RAIS MAGUFULI KUELEKEA SHEREHE ZA UHURU DESEMBA 9, 2018
link : SALAMU ZA RAIS MAGUFULI KUELEKEA SHEREHE ZA UHURU DESEMBA 9, 2018
SALAMU ZA RAIS MAGUFULI KUELEKEA SHEREHE ZA UHURU DESEMBA 9, 2018
zilizopita
*Asisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana kujenga uchumi wa nchi
yetu
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
RAIS wa Serikali ya Awamu ya Tano Dk.John Magufuli amewatakia Watanzania wote nchini kutafakari tulikotoka, tulipo na tunakokwenda huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kufanya kazi ili kujenga uchumi imara hasa kwa kuzingatia kwa sasa tupo kwenye vita ya kiuchumi ambayo lazima wote tushirikiane kuishinda.
Ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati anatoa salamu za kuwatakia kila laheri Watanzania katika kuelekea kuadhimisha miaka 57 ya Uhuru wa Tanganyika Desemba 9, 2018 ambapo itakuwa Jumapili ya wiki hii na kufafanua siku hiyo itakuwa ni ya mapumziko, ambayo itumike kutafakari tulikotoka na tunakokwenda.
"Kila laheri Watanzania katika kusherehekea miaka 57 ya Uhuru wa Tanganyika.Kama ambavyo mnafahamu tayari fedha Sh.bilioni moja
zilitengwa kwa ajili ya kufanikisha sherehe hizo lakini nimeshatoa maelekezo fedha hizo zitumike kujenga Hospitali Dodoma ambayo itaitwa Hospitali ya Uhuru,"amesema Rais Dk.Magufuli na kufafanua kwa kuwa Serikali inahamia Dodoma kuna umuhimu wa kujengwa kwa hospitali nyingine ili ziwepo mbili,"amesema.
Amesema kuwa tayari sehemu ya watumishi wa Serikali wapo Dodoma na amebaki yeye tu ambaye naye anajiandaa kuondoka siku za hivi karibuni na hivyo ndio maana ni muhimu kujengwa kwa hospitali ya pili ili isaidiane na Hospitali ya Mkapa.
Hivyo makala SALAMU ZA RAIS MAGUFULI KUELEKEA SHEREHE ZA UHURU DESEMBA 9, 2018
yaani makala yote SALAMU ZA RAIS MAGUFULI KUELEKEA SHEREHE ZA UHURU DESEMBA 9, 2018 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SALAMU ZA RAIS MAGUFULI KUELEKEA SHEREHE ZA UHURU DESEMBA 9, 2018 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/salamu-za-rais-magufuli-kuelekea.html
0 Response to "SALAMU ZA RAIS MAGUFULI KUELEKEA SHEREHE ZA UHURU DESEMBA 9, 2018"
Post a Comment