Loading...
title : DC SHINYANGA AFUNGUA KIKAO CHA TAHOSA, ATOA TAHADHARI KWA WAKUU WA SHULE
link : DC SHINYANGA AFUNGUA KIKAO CHA TAHOSA, ATOA TAHADHARI KWA WAKUU WA SHULE
DC SHINYANGA AFUNGUA KIKAO CHA TAHOSA, ATOA TAHADHARI KWA WAKUU WA SHULE
Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine MatiroMatiro amewatahadharisha wakuu wa shule za sekondari wilayani humo kutothubutu kuchangisha pesa kwa wazazi na wanafunzi kwa ajili ya mitihani ya shule na shule kwani ni kwenda kinyume cha agizo la rais John Pombe Magufuli linalokataza michango shuleni.
Matiro ametoa tahadhari hiyo leo Jumatano Februari 7,2018katika kikao cha kwanza kwa mwaka 2018 cha Umoja wa wakuu wa shule za sekondari Tanzania (TAHOSA) halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Vijijini) kilichofanyika katika ukumbi wa Mwalimu House Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wakuu wa shule 27 za sekondari zilizopo katika halmashauri hiyo.
Aidha aliwataka wakurugenzi wa halmashauri za wilaya kutumia mapato ya ndani na juhudi za wafadhili au wadau wa elimu kufanikisha mitihani ya wilaya badala ya kuchangisha wazazi na wanafunzi.
"Naomba mitihani mnayofanya ya Interschool Examination isihusishe michango yoyote kutoka kwa wazazi na wanafunzi, tukihusisha michango tunakuwa tumekwenda kinyume na kanuni, taratibu na matamko yanayotolewa na viongozi wetu”,alisisitiza .
"Hakikisheni pia pesa za serikali zinatumika kulingana na kanuni na utaratibu uliopangwa,zisipotumika vizuri maana yake mmeshindwa kufanya kazi mtawajibishwa”,alieleza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua kikao cha Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSA) halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Vijijini) . Kushoto ni mwenyekiti wa TAHOSA wa halmashauri hiyo Leonard Laurent. Kulia ni Kaimu mkurugezi wa halmashauri hiyo Stewart Makali.
Wakuu wa shule za sekondari katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Matiro aliwasisitiza wakuu hao wa shule kuwachukulia hatua watu wanaowapa mimba wanafunzi na kuhakikisha wanatoa elimu kuhusu madhara ya ndoa na mimba za utotoni.
Hivyo makala DC SHINYANGA AFUNGUA KIKAO CHA TAHOSA, ATOA TAHADHARI KWA WAKUU WA SHULE
yaani makala yote DC SHINYANGA AFUNGUA KIKAO CHA TAHOSA, ATOA TAHADHARI KWA WAKUU WA SHULE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC SHINYANGA AFUNGUA KIKAO CHA TAHOSA, ATOA TAHADHARI KWA WAKUU WA SHULE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/dc-shinyanga-afungua-kikao-cha-tahosa.html
0 Response to "DC SHINYANGA AFUNGUA KIKAO CHA TAHOSA, ATOA TAHADHARI KWA WAKUU WA SHULE"
Post a Comment