Loading...
title : Serikali yahimiza Usawa wa Jinsia
link : Serikali yahimiza Usawa wa Jinsia
Serikali yahimiza Usawa wa Jinsia
Na Mwandishi Wetu
Serikali imesisitiza uwepo wa usawa wa kijinsia katika sekta mbalimbali ili kuendelea kuunga jitihada za kuwezesha usawa huo ambao uliasisiwa katika Mkutano wa Nne wa Dunia wa Wanawake uliofanyika Beijing nchini China mwaka 1995 huku ikisisitiza ni muhimu kuundwa kwa madawati ya jinsia katika idara za serikali.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizindua Mtandao wa Wanawake na Utambulisho wa Sera ya Haki na Ulinzi wa Mtoto katika Jeshi la Magereza leo jijini Dar es Salaam .
Amesema Serikali imeweka mkazo katika kuhakikisha usawa wa kijnsia unafikiwa katika sekta na nyanja mbalimbali kwa kuchukua hatua ikiwemo kuandaliwa kwa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 pamoja na Mkakati wa Utekelezaji wake kwa lengo la kuweka mazingira muafaka na kuhakikisha kuwa masuala ya jinsia yanzingatiwa na wadau ikiwemo Wizara, Idara na Wakala za Serikali, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi na Wadau wa Maendeleo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), na Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mtandao wa Wanawake na Utambulisho wa Sera ya Haki na Ulinzi wa Mtoto katika Jeshi la Magereza. Uzinduzi huo umefanyika leo katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu(katikati) akimkabidhi tuzo Mwakilishi wa Benki ya NMB,ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa taasisi hiyo ya kifedha katika uanzishwaji wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza lililozinduliwa katika Viwanja vya Karimjee,leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu(katikati), akimkabidhi tuzo mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Wanawake(TAWLA), ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa taasisi hiyo katika uanzishwaji wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza lililozinduliwa katika Viwanja vya Karimjee,leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akiangalia bidhaa inayotengenezwa na Jeshi la Magereza wakati alipotembelea mabanda ya jeshi hilo wakati wa Uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza lililozinduliwa katika Viwanja vya Karimjee, leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na Jeshi la Magereza wakati alipotembelea mabanda ya jeshi hilo wakati wa Uzunduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza lililozinduliwa katika Viwanja vya Karimjee,leo jijini Dar es Salaam..Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Serikali yahimiza Usawa wa Jinsia
yaani makala yote Serikali yahimiza Usawa wa Jinsia Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali yahimiza Usawa wa Jinsia mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/serikali-yahimiza-usawa-wa-jinsia.html
0 Response to "Serikali yahimiza Usawa wa Jinsia"
Post a Comment