Loading...

SERIKALI YATOA MAFUNZO RASMI KWA MAFUNDI SIMU ZA MKONONI NCHINI

Loading...
SERIKALI YATOA MAFUNZO RASMI KWA MAFUNDI SIMU ZA MKONONI NCHINI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YATOA MAFUNZO RASMI KWA MAFUNDI SIMU ZA MKONONI NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YATOA MAFUNZO RASMI KWA MAFUNDI SIMU ZA MKONONI NCHINI
link : SERIKALI YATOA MAFUNZO RASMI KWA MAFUNDI SIMU ZA MKONONI NCHINI

soma pia


SERIKALI YATOA MAFUNZO RASMI KWA MAFUNDI SIMU ZA MKONONI NCHINI

Naibu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Jim Yonazi ametoa vyeti vya mafunzo ya muda mfupi kwa mafundi simu za mkononi waliohitimu mafunzo hayo kwenye Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe
“Nawapongeza mafundi simu wa kike watatu kwa kuwa suala la ufundi linachukuliwa kuwa ni la wanaume, naamini ninyi watatu mtakuwa chachu kwa wanawake wengine kujiunga na mafunzo haya,” amesema Dkt. Yonazi wakati akitoa vyeti kwa mafundi simu za mkononi 68 waliohitimu mafunzo hayo ambapo kati yao watatu ni wanawake waliohudhuria mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Julai mwaka huu. Ameongeza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa mafundi simu za mkononi kwa kuwa yatawawezesha kulinda usalama wa taarifa, yataleta tija na kuweza kuingiza fedha za kigeni kupitia Sekta ya Mawasiliano. 
Amefafanua kuwa mafunzo hayo yako sambamba na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambapo Serikali imejipanga kutekeleza Ilani hiyo kupitia kauli mbiu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya ujenzi wa viwanda ambapo tayari Kampuni ya IPP Touchmate Tanzania Ltd itajenga kiwanda cha simu za mkononi nchini na wako tayari kuwapa ajira wahitimu hao kwa kuwa ni mafundi simu wa kwanza nchini kupata mafunzo hayo rasmi
Naibu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Jim Yonazi (wa kwanza kulia) akikabidhi cheti kwa Mwanahamis Abdul Salim aliyehitimu mafunzo ya kutengeneza simu za mkononi kwenye Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT). Anayeshuhudia wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara hiyo, Mulembwa Munaku
Naibu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Jim Yonazi (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na mafundi simu za mkononi wa kike watatu (waliosimama) kati ya 68 waliohitimu mafunzo DIT, Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa TEHAMA, Wizara hiyo Mulembwa Munaku na wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkuu wa Taasisi ya DIT, Prof. Patrick Nsimama 
Naibu Katibu Mkuu Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Jim Yonazi (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na meza kuu na wadau waliohudhuria hafla ya utoaji vyeti na leseni kwa mafundi simu za mkononi wa kwanza waliohitimu mafunzo yao, Taasisi ya DIT, Dar es Salaam. Wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara hiyo Mulembwa Munaku na wa pili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Taasisi ya DIT, Prof. Patrick Nsimama
Naibu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Jim Yonazi (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na mafundi simu za mkononi waliohitimu mafunzo hayo kwenye Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam na baadhi ya wadau wa Sekta hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Hivyo makala SERIKALI YATOA MAFUNZO RASMI KWA MAFUNDI SIMU ZA MKONONI NCHINI

yaani makala yote SERIKALI YATOA MAFUNZO RASMI KWA MAFUNDI SIMU ZA MKONONI NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YATOA MAFUNZO RASMI KWA MAFUNDI SIMU ZA MKONONI NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/serikali-yatoa-mafunzo-rasmi-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI YATOA MAFUNZO RASMI KWA MAFUNDI SIMU ZA MKONONI NCHINI"

Post a Comment

Loading...