Loading...
title : UJENZI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA MUSOMA WAENDELEA KWA KASI
link : UJENZI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA MUSOMA WAENDELEA KWA KASI
UJENZI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA MUSOMA WAENDELEA KWA KASI
Na Benny Mwaipaja, WFM, Musoma
WAKAZI wa mkoa wa Mara wanatarajia kuondokana na adha ya kufuata huduma za Mahakama Kuu mkoani Mwanza, umbali wa zaidi ya kilometa 200 kutoka mjini Musoma, baada ya ujenzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma kukaribia kukamilika mapema mwakani.
Wakizungumza na timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, baadhi ya wakazi wa mji wa Musoma Mary Mohamed na Happy Mjito, wamesema kuwa hivi sasa wanatumia fedha nyingi kufuatilia haki zao Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza hali inayowafanya wengi wao kukata tamaa kufuatilia kesi zao hivyo kupoteze haki zao
"Ukikata rufaa ya kesi unaambiwa uende Mwanza wakati hata Mahakama Kuu yenyewe ya Kanda ya Mwanza hatuijui mahali ilipo, sasa tunafurahi kwamba tutakuwa tumiendesha kesi zetu hapa hapa Musoma" alisema Bi. Happy Mjito
Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, wakipata maelezo na ufafanuzi mbalimbali kutoka msimamizi wa Ujenzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Mhandisi Uday Dadrawalla (kulia) walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzo wa Miundombinu ya Mahakama hiyo unaosimamiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania.
Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, wakipata maelezo na ufafanuzi mbalimbali kutoka msimamizi wa Ujenzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Mhandisi Uday Dadrawalla (kulia) walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Miundombinu ya Mahakama hiyo unaosimamiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania kwa gharama ya shilingi bilioni 6.2.
Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, Maafisa wa Mahakama Kuu-Musoma na Wakandarasi wa Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, wakinyanyua kofia za usalama baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa Mahakama hiyo uliofikia asilimia 80 na umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 6.2
Mwonekano wa Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Musoma ambalo ujenzi wake unaendelea na umefikia asilimia 80 na unatarajia kukamilika ifikapo mwezi April, 2019, kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 6.2.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala UJENZI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA MUSOMA WAENDELEA KWA KASI
yaani makala yote UJENZI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA MUSOMA WAENDELEA KWA KASI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UJENZI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA MUSOMA WAENDELEA KWA KASI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/ujenzi-wa-mahakama-kuu-kanda-ya-musoma_17.html
0 Response to "UJENZI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA MUSOMA WAENDELEA KWA KASI"
Post a Comment