Loading...
title : TAMASHA LA MAPINDUZI FESTIVAL LAZINDULIWA
link : TAMASHA LA MAPINDUZI FESTIVAL LAZINDULIWA
TAMASHA LA MAPINDUZI FESTIVAL LAZINDULIWA
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MABINGWA wa burudani ya muziki wa kizazi kipya visiwani Zanzibar jana wameonyesha uwezo wao katika kuiwakilisha vyema sanaa ya muziki nchini. Wasanii hao wamezitumia vyema sauti, kumiliki jukwaa pamoja na kucheza na hisia kali za mashabiki waliobobea katika uwanja wa burudani ambapo yote hayo yalionekana kwa kila msanii aliyepanda kuimba katika Tamasha hilo la 'Safari ya muziki miaka 55 Mapinduzi' .
Akizindua Tamasha hilo Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Zanzibar Bimkubwa Sukwa katika Uwanja wa Mpendae Shule ya Sekondari Wilaya ya Mjini , aliitaka jamii kuunga mkono juhudi za wasanii wa kizazi kipya waliojitolea kwenda kwa wananchi kujitangaza na kuonyesha vipaji vyao.
Alisema umefika muda mwafaka wa Serikali na wadau mbali mbali wa maendeleo ndani na nje ya Zanzibar kuwa mstari wa mbele kusaidia juhudi za wasanii kwani sanaa ya muziki ni sehemu pana ya vijana wengi kujiajiri wenyewe. Katika maelezo yake Naibu Mstahiki Meya, alieleza kuwa tamasha limebeba tunu ya nchi ambayo ni Mapinduzi ya miaka 55 jambo ambalo wasanii hao wameonyesha uzalendo wa kweli wa kuenzi falsafa ya Mapinduzi.

Wasanii mbali mbali wa muziki wa kizazi kipya wakionyesha uwezo wao wa kuteka jukwaa huko katika Tamasha la Safari ya Muziki Mapinduzi Festival lililozinduliwa jana katika Jimbo la Mpendae Wilaya ya Mjini Zanzibar.
NAIBU Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mjini Bimkubwa Sukwa akikagua Timu ya Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya waliocheza na Timu ya Mpendae ikiwa ni sehemu ya wasanii kuwa karibu na jamii.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPAHivyo makala TAMASHA LA MAPINDUZI FESTIVAL LAZINDULIWA
yaani makala yote TAMASHA LA MAPINDUZI FESTIVAL LAZINDULIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAMASHA LA MAPINDUZI FESTIVAL LAZINDULIWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/tamasha-la-mapinduzi-festival.html
0 Response to "TAMASHA LA MAPINDUZI FESTIVAL LAZINDULIWA"
Post a Comment