Loading...

UPANUZI WA BANDARI GATI NAMBA MOJA WAFIKIA ASILIMIA 100

Loading...
UPANUZI WA BANDARI GATI NAMBA MOJA WAFIKIA ASILIMIA 100 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UPANUZI WA BANDARI GATI NAMBA MOJA WAFIKIA ASILIMIA 100, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UPANUZI WA BANDARI GATI NAMBA MOJA WAFIKIA ASILIMIA 100
link : UPANUZI WA BANDARI GATI NAMBA MOJA WAFIKIA ASILIMIA 100

soma pia


UPANUZI WA BANDARI GATI NAMBA MOJA WAFIKIA ASILIMIA 100

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam umefikia hatua nzuri baada ya kukamilka kwa upanuzi wa gati namba moja kwa asilimia 100 huku meli ya kwanza ikitarajiwa kutia nanga wiki moja ijayo ikishuhudiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano.

Hayo yameelezwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mhandisi Deusdediti Kakoko, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi wa Sh. bilioni 336.7 wa upanuzi wa bandari hiyo.

Amesema upanuzi huo umeiongezea uwezo gati hiyo yenye urefu wa mita 192 wa kubeba meli kubwa mbili za tani 45,000 hadi tani 60,000 kwa wakati mmoja kutokana na kuongezewa kitako cha upana wa mita 11.5 kinachobebwa na nguzo imara za zege zilizochimbiwa mita 70 chini ya bahari.

Amesema baada ya mkandarasi kukabidhi gati hiyo siku chache zijazo atakabidhiwa na kuanza kazi ya upanuzi wa gati namba mbili inayotarajiwa kukamilika Machi mwakani na upanuzi utaendelea hadi kufikia gati namba saba.

Akizungumzia ujenzi wa gati ya magari (RoRo Berth) pamoja na yadi ya kuegesha magari amesema mradi huo ulitakiwa uwe umekamilika lakini mkandarasi alikutana na changamoto ya kuwepo kwa udogo mbaya na hivyo kulazimika kutafuta udogo mzuri na kuujaza na kwamba ujenzi unatarajiwa kukamilika na kukabidhiwa Juni mwakani.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mhandisi Deusdediti Kakoko, akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya mradi wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Fredy Lihundi, akifafanua jambo
Wakandarasi wanaofanya upanuzi katika Bandari ya Dar es Salaam, wakijadili jambo katika mradi huo na viongozi wa TPA.
Mtambo wa kuchimba kina cha Bahari ukimwaga mchanga nje ya bahari katika Bandari ya Dar es Salaam.



Hivyo makala UPANUZI WA BANDARI GATI NAMBA MOJA WAFIKIA ASILIMIA 100

yaani makala yote UPANUZI WA BANDARI GATI NAMBA MOJA WAFIKIA ASILIMIA 100 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UPANUZI WA BANDARI GATI NAMBA MOJA WAFIKIA ASILIMIA 100 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/upanuzi-wa-bandari-gati-namba-moja.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "UPANUZI WA BANDARI GATI NAMBA MOJA WAFIKIA ASILIMIA 100"

Post a Comment

Loading...