Loading...
title : WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR KUYAFUNGIA MACHINJIO YASIYO NA VIWANGO
link : WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR KUYAFUNGIA MACHINJIO YASIYO NA VIWANGO
WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR KUYAFUNGIA MACHINJIO YASIYO NA VIWANGO
Na Khadija Khamis –Maelezo
Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) imeahidi kusimamia na kudhibiti ubora wa machinjio ya ng’ombe na yatakayobainika hayana kiwango cha kufanya kazi hiyo yatafungiwa ili kuhakikisha wananchi wanapata chakula kilicho salama kwa afya zao.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea machinjio ya Kinyasini,Donge Muwanda na Mahonda katika Mkoa wa Kaskazini Unguja kuangali mazingira na ubora wa machinjio hayo.
Amesema juhudi za Serikali kupitia Wakala wa Chakula na Dawa ni kuhakikisha wananchi wanapata chakula kilichoandaliwa katika ubora unaostahiki ambao utamlinda mtumiaji asipatwe na madhara.
Alisema Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar walianzisha kanuni ya kuwataka wananchi wanaosafirisha nyama ya ngombe kwa ajili ya biashara kutumia gari maalum za kusafirisha kutoka machinjioni kwa lengo la kulinda usalama wa chakula hicho
Dkt. Khamis amezitaka taasisi zinazosimamia suala la uingizaji wa ngombe ikiwemo Idara ya Mifugo, na Kilimo Wakaguzi pamoja na vyombo vya ulinzi kuwa na mashirikiano ya pamoja ili kuhakikisha ngombe hawachinjwi katika mazingira hatarishi.
Diwani wa Wadi ya Mahonda Haji Fadhil Mkadam amewaomba Wakala wa Chakula na Dawa kuwasaidia kumaliza ujenzi wa chinjio lao liweze kuanza kazi ili kuepuka usumbufu na kuvunja sheria ya kuchinja ngombe katika sehemu zisizorasmi.
Kaimu Mkurugenzi Wakala wa Chakula na Dawa Dkt Khamis Ali na Mkaguzi wa Chakula Dkt. Faki Mohd Haji wakikagua Chinjio la Kinyasini linalomilikwa na Abdalla Mohd walipofanya ziara ya kuangalia mazingira ya machinjio ya mkoa Kusini Unguja.
Mmiliki wa Chinjio la Kinyasini Abdalla Mohd akiwaeleza wakaguzi juhudi anazochukua katika kuhakikisha mazingira ya sehemu yake ya kazi yanakuwa salama na wananchi wanapata kitoweo kilicho bora kwa afya zao
Wakaguzi wa Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Khamis Ali wakiangalio chinjiola kisasa la Donge Muwanda walipofanya ziara ya kuangalia hali ya mazingira ya machinjio ya Mkoa Kaskazini Unguja.
Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Chakula na Dawa Dkt. Khamis Ali akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara ya kukagua machinjio matatu ya Mkoa Kaskazini Unguja.PICHA NA RAMADHANI ALI - MAELEZO ZANZIBAR
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR KUYAFUNGIA MACHINJIO YASIYO NA VIWANGO
yaani makala yote WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR KUYAFUNGIA MACHINJIO YASIYO NA VIWANGO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR KUYAFUNGIA MACHINJIO YASIYO NA VIWANGO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/wakala-wa-chakula-na-dawa-zanzibar.html
0 Response to "WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR KUYAFUNGIA MACHINJIO YASIYO NA VIWANGO"
Post a Comment