Loading...
title : WANAFUNZI CHUO CHA UTALII WATUNUKIWA VYETI.
link : WANAFUNZI CHUO CHA UTALII WATUNUKIWA VYETI.
WANAFUNZI CHUO CHA UTALII WATUNUKIWA VYETI.
Wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii ambao wamehitimu mafunzo ya utalii na ukarimu wametakiwa kwenda kufanyakazi kwa bidii na nidhamu ili waweze kuwa mabalozi bora wa chuo hicho.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ametoa wito huo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 16 ya Chuo hicho ambayo yamefanyika kwenye kampasi ya Bustani jijini hapa.
Mhe.Kanyasu amesema sekta ya utalii ndiyo yenye ushindani mkubwa hapa nchini hivyo itakapoendelezwa itasaidia kuondoa tatizo la umaskini.
Aidha amesema serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha mpaka kufika mwaka 2020 waweze kufikisha jumla ya watalii Mill.2.
"Nilazima kuhakikisha kuwa chuo kinafanya juhudi kubwa kushirikiana na wadau binafsi ili wahitimu wetu wawe wamebobea katika taaluma yao"amesema Mhe Kanyasu
Awali akitoa hutuba kwenye mahafali hayo Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Dkt.Shogo Mlozi amesema jukumu lao ni kuhakikisha wanazalisha wahitimu wanaoendana na soko la kimataifa.
"Leo tunafuraha kwa kuwa tunawanajenzi 89 wakiwemo 51 kutoka kampasi ya Arusha na 38 kutoka kampani ya Bustani ambao wanatunukiwa vyeti vyao katika ngazi ya astashahada sanjari na wahitimu wengine wa chuo hicho"amesema Dkt Shogo
Katika hatua nyingine amesema licha ya chuo hicho kuwa na mafanikio kwa wanafunzi kufanya kazi katika maeneo tofauti nchini na nje ya nchi bado wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya uhaba wa madarasa kwa kampasi ya Arusha na Temeke pamoja na uhaba wa wafanyakazi na mabweni ya wanafunzi.
Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Albert Orkel amesema watahakikisha wananendelea kushirikiana na chuo hicho ili kiendelee kutoa mafunzo bora kwa wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi ambao wamehitimu hii leo wamesema mafunzo ambayo wameyapata kwenye chuo hicho yamewasaidia kufanya kazi kwa uadilifu lakini pia yamewajengea uwezo wa kujiajiri wenyewe.
Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) ni wakala uliopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wenye dhamana ya kutoa mafunzo ya ukarimu na utalii nchini lakini pia kinatoa ushauri wa kufanya tafiti katika fani ya ukarimu na utalii
Hivyo makala WANAFUNZI CHUO CHA UTALII WATUNUKIWA VYETI.
yaani makala yote WANAFUNZI CHUO CHA UTALII WATUNUKIWA VYETI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI CHUO CHA UTALII WATUNUKIWA VYETI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/wanafunzi-chuo-cha-utalii-watunukiwa.html
0 Response to "WANAFUNZI CHUO CHA UTALII WATUNUKIWA VYETI."
Post a Comment