Loading...

Waziri Mhagama aitaja Mikoa 11 vinara kwa Mabaraza ya Biashara

Loading...
Waziri Mhagama aitaja Mikoa 11 vinara kwa Mabaraza ya Biashara - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Waziri Mhagama aitaja Mikoa 11 vinara kwa Mabaraza ya Biashara, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Waziri Mhagama aitaja Mikoa 11 vinara kwa Mabaraza ya Biashara
link : Waziri Mhagama aitaja Mikoa 11 vinara kwa Mabaraza ya Biashara

soma pia


Waziri Mhagama aitaja Mikoa 11 vinara kwa Mabaraza ya Biashara

Na OWM, Kigoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), ameitaja mikoa 11 ambayo ilianzisha mabaraza ya Biashara na hadi sasa yako hai na kubainisha kuwa mikoa mingine ilitekeleza agizo la kuanzisha mabaraza hayo tu lakini utendaji wa Mabaraza hayo umekuwa siyo endelevu.

Waziri Mhagama ameitaja Mikoa hiyo 11 ambayo Mabaraza yake yako hai hadi sasa kuwa ni Dodoma, Kigoma, Tanga, Geita, Morogoro, shinyanga, Dar es Salaam, Pwani, Iringa, Songwe na Mbeya. Aidha, Mhagama amebainisha kuwa Mikoa mingine ambayo mabaraza yake hayafanyi vikao inakiuka Waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 2001 unaosisitiza kuanzishwa kwa mabaraza hayo na utendaji wake kuwa endelevu.

Akiongea wakati wa kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Taifa la Biashara mkoani Kigoma, Waziri Mhagama alifafanua kuwa Dhumuni kuu la kuanzisha mabaraza ya biashara hususani katika ngazi ya wilaya na mikoa ni kuweka mfumo rasmi wa kuwakutanisha viongozi wakuu wa Serikali na Sekta Binafsi katika kila ngazi ya utawala, kujadiliana jinsi ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa ajili ya kukuza sekta binafsi ambayo ndio muhimili muhimu wa kukuza uchumi wa nchi.

“Hatuwezi kuwa tunamshuhudia Mhe. Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli anaitisha vikao vya Baraza la Taifa la Biashara katika ngazi ya Taifa lakini katika ngazi ya mkoa na wilaya hamtekelezi maagizo hayo, lazima mabaraza yakutane ili kutatua kero za wafanyabiashara na wawekezaji katika ngazi ya mkoa na wilaya, lakini pia itasaidia kuibua fursa za uwekezaji na kuzinadi fursa hizo, na sisi tumeamua kukagua mkoa mmoja baada ya mwingine ili kupunguza kero za wafanya biashara na wawekezaji” Amesema Mhagama

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akisisitiza jambo wakati alipokutana na wajumbe wa Baraza la Biashara Mkoa wa Kigoma, wakati alipofika mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Taifa, kulia kwake ni Mkuu wa mkoa huo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga, Katibu Tawala wa mkoa huo, Rashid Mchata na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson Anga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa Kigoma, Rashid Mchata, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Baraza la Biashara la mkoa huo, wakati Waziri alipofika mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Taifa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (LIC), Andrew Mhina akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo mkoani Kigoma, wakati Waziri alipofika mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Taifa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akiongea na Mjasiriamali aliyekuwa akihudumiwa katika kituo cha Biashara (One Stop Business Center) wilayani Kigoma, wakati alipofika mkoani Kigoma kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Taifa.



Hivyo makala Waziri Mhagama aitaja Mikoa 11 vinara kwa Mabaraza ya Biashara

yaani makala yote Waziri Mhagama aitaja Mikoa 11 vinara kwa Mabaraza ya Biashara Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Mhagama aitaja Mikoa 11 vinara kwa Mabaraza ya Biashara mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/waziri-mhagama-aitaja-mikoa-11-vinara.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Waziri Mhagama aitaja Mikoa 11 vinara kwa Mabaraza ya Biashara"

Post a Comment

Loading...