Loading...

WAZIRI WA KILIMO AAGIZA VYUO VIKUU KUTANGAZA MATOKEO YA TAFITI ZAO

Loading...
WAZIRI WA KILIMO AAGIZA VYUO VIKUU KUTANGAZA MATOKEO YA TAFITI ZAO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI WA KILIMO AAGIZA VYUO VIKUU KUTANGAZA MATOKEO YA TAFITI ZAO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI WA KILIMO AAGIZA VYUO VIKUU KUTANGAZA MATOKEO YA TAFITI ZAO
link : WAZIRI WA KILIMO AAGIZA VYUO VIKUU KUTANGAZA MATOKEO YA TAFITI ZAO

soma pia


WAZIRI WA KILIMO AAGIZA VYUO VIKUU KUTANGAZA MATOKEO YA TAFITI ZAO

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Kilimanjaro

Imebainika kuwa tafiti na machapisho mengi yanayofanywa na wanataaluma na wanafunzi katika Vyuo mbalimbali si tu zinasaidia kujenga taswira za vyuo bali zinapaswa kuwa sehemu ya kufanya elimu iwe nzuri na bora zaidi.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 6 Disemba 2018 wakati akizungumza kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.

Mhe Hasunga amewaagiza watendaji wa Chuo hicho sambamba na vyuo vingine nchini kufanya tafiti za kutosha katika tasnia ya ushirika na kuhakikisha kuwa Matokeo ya tafiti hizo yanawafikia walengwa. "Serikali nayo kwa upande wake imeweka na itaendelea kuweka mazingira rafiki zaidi yatakayosaidia kuimarisha dhana ya ushirika miongoni mwa jamii ya watanzania" Alisema

Alisisitiza kuwa moja ya kadhia inayovikumba vyuo mbalimbali nchini ni kutowekwa wazi kwa haraka machapisho na Tafiti mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutangaza ili zijulikane katika sehemu mbalimbali Duniani.

"Ndugu zangu hakuna nchi inaweza kuendelea bila kuwekeza kwenye utafiti hivyo ni lazima kuongeza jitihada na juhudi katika utafiti" Alisisitiza.Alisema kuwa Vyuo vikuu vinatambuliwa kama taasisi zilizobobea katika kufundisha, kujifunzia, kufanya tafiti na kutoa huduma za ushauri hivyo vinapaswa kutangaza matokeo ya Tafiti wanazozifanya.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi zawadi ya mwanafunzi bora kitaaluma ngazi ya Stashahada ya Uhasibu na Uongozi Ndg Methusela Piniel kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tarehe 6 Disemba 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi zawadi ya mwanafunzi bora kitaaluma ngazi ya Shahada ya Biashara na Uchumi Bi Diana Kibodya kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tarehe 6 Disemba 2018.
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Prof Faustine K. Bee akitoa taarifa ya chuo hicho kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tarehe 6 Disemba 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi sambamba na baadhi ya wahitimu kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma chuoni hapo tarehe 6 Disemba 2018.



Hivyo makala WAZIRI WA KILIMO AAGIZA VYUO VIKUU KUTANGAZA MATOKEO YA TAFITI ZAO

yaani makala yote WAZIRI WA KILIMO AAGIZA VYUO VIKUU KUTANGAZA MATOKEO YA TAFITI ZAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI WA KILIMO AAGIZA VYUO VIKUU KUTANGAZA MATOKEO YA TAFITI ZAO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/waziri-wa-kilimo-aagiza-vyuo-vikuu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI WA KILIMO AAGIZA VYUO VIKUU KUTANGAZA MATOKEO YA TAFITI ZAO"

Post a Comment

Loading...