Loading...
title : AZAM FC YAJIZATITI KUONDOKA NA ALAMA TATU SOKOINE
link : AZAM FC YAJIZATITI KUONDOKA NA ALAMA TATU SOKOINE
AZAM FC YAJIZATITI KUONDOKA NA ALAMA TATU SOKOINE
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KIKOSI cha Azam kimejidhatiti kufanya kweli kwenye mchezo ujao dhidi ya Tanzania Prison baada ya kutoka katika mchezo wake dhidi ya Lipuli uliomalizika kwa kupata sare ya bao 1-1.
Kocha Msaidizi wa Azam, Juma Mwambusi, aliwapongeza wachezaji kwa kutoka nyuma na hatimaye kupata sare ya ugenini.
“Mchezo ulikuwa ni mzuri na mgumu, Azam kipindi cha kwanza hatukuweza kucheza vizuri kwa sababu wachezaji waliingia kwenye mchezo wakiwa na kasi ya chini, kwa kiasi kikubwa ilichangiwa na hali ya uwanja kwa sababu ilinyesha mvua kabla ya mpira kuanza kwa hiyo walicheza kwa tahadhari zaidi ili wasiweze kupata majeraha na kusababisha matatizo langoni,” alisema.
Alisema waliweza kufanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kucheza mpira wa kushambulia kutokea pembeni na katikati hadi kufanikiwa kusawazisha bao wailotanguliwa kipindi cha kwanza na Lipuli.
“Pengine tungeweza kutulia zaidi kwa washambuliaji wetu tungeweza kushinda mabao mawili au matatu na kuondoka na pointi tatu katika mechi hii, yote kwa yote tunajipanga kwa mchezo unaokuja (Tanzania Prisons,” alisema.
Matokeo dhidi ya Lipuli yameifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 49 ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikizidiwa pointi tisa na vinara Yanga waliokuwa nazo 58, lakini matajiri hao wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Hivyo makala AZAM FC YAJIZATITI KUONDOKA NA ALAMA TATU SOKOINE
yaani makala yote AZAM FC YAJIZATITI KUONDOKA NA ALAMA TATU SOKOINE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AZAM FC YAJIZATITI KUONDOKA NA ALAMA TATU SOKOINE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/azam-fc-yajizatiti-kuondoka-na-alama.html
0 Response to "AZAM FC YAJIZATITI KUONDOKA NA ALAMA TATU SOKOINE"
Post a Comment