Loading...

DIGITALI KWA MAENDELEO (OXFAM) YAIBUA CHANGAMOTO KWA JAMII NYINGI IKIWEMO YA MAJI

Loading...
DIGITALI KWA MAENDELEO (OXFAM) YAIBUA CHANGAMOTO KWA JAMII NYINGI IKIWEMO YA MAJI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DIGITALI KWA MAENDELEO (OXFAM) YAIBUA CHANGAMOTO KWA JAMII NYINGI IKIWEMO YA MAJI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DIGITALI KWA MAENDELEO (OXFAM) YAIBUA CHANGAMOTO KWA JAMII NYINGI IKIWEMO YA MAJI
link : DIGITALI KWA MAENDELEO (OXFAM) YAIBUA CHANGAMOTO KWA JAMII NYINGI IKIWEMO YA MAJI

soma pia


DIGITALI KWA MAENDELEO (OXFAM) YAIBUA CHANGAMOTO KWA JAMII NYINGI IKIWEMO YA MAJI

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo akijibu akizungumza na waraghabishi kutoka mikoa mbalimbali katika mkutano wa Digitali kwa maendeleo ulioandaliwa na Shirika la OxfamTanzani na kufanyika Katika ukumbi wa  African Dreams Jijini Dodoma
Naibu waziri wa Elimu William  Olenasha akizungumza katika mkutano wa Waraghabishi wa Digitali kwa Maendeleo ulioandaliwa na Shirika la. OXFAM Tanzani Jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Elimu  Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Ngorongoro William Olenasha akipita taarifa kupitia simu yake ya mkononi katika mkutano wa Digitali kwa Maendeleo ulioandaliwa na Shirika la Oxfam Jijini Dodoma
Sabore Ngarusi Kutoka wilayani Ngorongoro akiuliza swali kwa Katibu Mkuu wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo kwamba wizara hiyo imejipangaje kuondoa taizo la maji wilayani humo.
 Mbunge wa Viti maalum Dodoma Mhe. Fatuma Tawfiq akifuatilia mjadala  katika mkutano huo wa Digitali kwa Maendeleo Jijini Dodoma
 Mbunge wa Mbogwe mkoa wa Geita  Mhe. Maselle akifuatilia mjadala kwa makini
 Mbunge wa Mtwara vijijini Mhe. Hawa Ghasia akichangia mjadala katika Mkutano wa Digitali kwa Maendeleo ulioandaliwa na Shirika la Oxfam Nchini Jijini Dodoma
 Mbunge wa Viti maalum Dodoma Mhe. Fatuma Tawfiq akichangia mada katika mkutano huo wa Digitali kwa Maendeleo Jijini Dodoma
 Katibu mkuu Wizara ya maji Profesa Kitila Mkumbo akifuatilia mjadala Digitali kwa Maendeleo kwa makini Jijini Dodoma
Jimmy Luhende Kutoka Shirika la ADLG. akichangia mada katika mkutano wa waraghabishi wa Digital Kwa maendeleo ulioandaliwa na Shirika la Oxfam Tanzania. 
Naibu Waziri wa Elimu Williwm Olenasha akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi kutoka katika Shirika la Oxfam Tanzania
Naibu waziri wa Elimu Willium Tate Ollenasha akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na Waandishi wa habari za mtandaoni Jijini Dodoma katika Mkutano wawaraghabishi Digitali kwa maendeleo

Na. Vero Ignatus, Dodoma

Zaidi ya 30% ya miradi ya maji iliyokamilika vijijini haifanyi kazi kwasababu imekabidhiwa kwa jamii kwani ni tofailuti na ile ya mijini ambayo inakabidhiwa kwa Wahandisi au kwa wataalamu wa maji

Hayo yamesemwa na Katibu mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo alipokuwa katika mkutano wa waraghabishi Digitali kwa maendeleo Jijini Dodoma ulioandaliwa na Shirika la Oxfam Nchini ambapo amesema miradi hiyo inapokabidhiwa kwa wananchi haina uangalizi wa kutosha

Profesa Mkumbo amesema Kituo kimoja Cha maji kinapaswa kuhudumia watu 250 hadi kufikia January 2019 tayari wameshajenga  vituo 130,000 vijijini na vinavyofanya kazi,83,000 takribani wananchi 60 mpaka 65 wanapata maji.

Amesema kuwa Madhumuni ya Sheria Mpya ya Rasilimali za Maji Na. 11/2009 ni kuhakikisha kuwa Rasilimali za Maji hapa nchini zinatunzwa, zinatumiwa, zinaendelezwa, zinaboreshwa, zinasimamiwa na kudhibitiwa kwa kuzingatia kanuni

Amesema kuwa Sheria mpya ya Maji iliyo pitishwa inagusia vipengele viwili uanzishwaji wa wakala wa maji vijijini adhabu kwa watu wanao haribu miundombinu ya maji

Amezitaja Wilaya ya Ngorongoro iliyopo mkoani Arusha  kuwa ni  mojawapo  yenye changamoto kubwa ya kufikiwa kutokana na Jiografia yake ila hadi sasa (Mb)Mh.William Ollenasha Ameshafanya usanifu vijiji 8 vitanufaika na mradi  wa maji

Akijibu swali lililoulizwa na mmoja wa Waraghabishi kuhisiana na  uondoshwaji wa bei za maji Profesa Mkumbo amesema Mchakato wa kupandisha bei ya maji ni shiriki, linaanza na mamlaka ya maji na mara nyingi upandaji wa bei ya maji inategemeana na gharama za uendeshwaji wa mamlaka za maji

Vilevile ameainisha Takwimu za upatikanaji wa maji kwamba zinazipata kwa aina mbili ambazo ni Miundombinu ya maji ilivyo sambazwa, Kutumia water system kwenye mtandao wa EWURA ambapo Tafiti yake hufanyika kwa kuwapigia wananchi na kuwauliza maswali

'' Kwa mujibu wa Takwimu za mwaka 2017 za NBS zinaonesha 66% ya wananchi wa Tanzania wanapata maji'' Alisema Mkumbo

Kwa upande wake Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Yeknolojia na mbunge wa Ngorongoro Willium Olenasha amelishukuru Shirika la Oxfam kwa kutoa mafunzo kwa wananchi namna ya kutumia nyenzo za digitali ili kuleta maendeleo kwa jamii inayowazunguka.

Naibu Waziri wa wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Olenasha amesema kuwa Serikali ipo pamoja na Oxfam pamoja na Waraghabishi katika kuhakikisha kwamba changamoto zinazoibuliwa na wananchi zinatatuliwa na viongozi husika kwa haraka na kwa wakati.

Ameongeza kuwa Nchi nyingi zimesonga mbele kwa kasi kwa sababu ya kutumia teknolojia ya dijitali hivyo Oxfam imekua ikishirikiana na serikali katika shughuli za maendeleo ikiwemo mradi huo wa Dijitali Kwa Maendeleo

Wakishukuru Shirika la Oxfam kwa mafunzo ya kutumia nyenzo za Digitali kwa maendeleo Lucy Samweli, Diwani viti Maalumu Kata ya Nyasato Geita amesema Kwa kutumia mitandao ya kijamii amepata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali wanaosoma anachokituma katika mitandao hiyo na hivyo kuboresha utendaji kazi yake

Na Bi Royce Jumanne, Mraghabishi kutoka Kigoma amesema kuwa  Kupitia simu zao za mkononi waraghabishi wamefanikiwa kuhamasisha jamii kuchangia madawati ili kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri.



Hivyo makala DIGITALI KWA MAENDELEO (OXFAM) YAIBUA CHANGAMOTO KWA JAMII NYINGI IKIWEMO YA MAJI

yaani makala yote DIGITALI KWA MAENDELEO (OXFAM) YAIBUA CHANGAMOTO KWA JAMII NYINGI IKIWEMO YA MAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DIGITALI KWA MAENDELEO (OXFAM) YAIBUA CHANGAMOTO KWA JAMII NYINGI IKIWEMO YA MAJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/digitali-kwa-maendeleo-oxfam-yaibua.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DIGITALI KWA MAENDELEO (OXFAM) YAIBUA CHANGAMOTO KWA JAMII NYINGI IKIWEMO YA MAJI"

Post a Comment

Loading...