Loading...

UKOSEFU WA MAENEO YA KILIMO UNACHANGIA LISHE DUNI MISENYI

Loading...
UKOSEFU WA MAENEO YA KILIMO UNACHANGIA LISHE DUNI MISENYI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UKOSEFU WA MAENEO YA KILIMO UNACHANGIA LISHE DUNI MISENYI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UKOSEFU WA MAENEO YA KILIMO UNACHANGIA LISHE DUNI MISENYI
link : UKOSEFU WA MAENEO YA KILIMO UNACHANGIA LISHE DUNI MISENYI

soma pia


UKOSEFU WA MAENEO YA KILIMO UNACHANGIA LISHE DUNI MISENYI

Anaandika Abdullatif Yunus – Misenyi, Kagera. 

Kufuatia Uzinduzi wa Kampeni ya Lishe na Usindikaji kwa maeneo yaliyokumbwa na majanga Mbali mbali Wilayani Misenyi, imegundulika kuwa sababu nyingine inayopelekea uwepo wa lishe duni kwa baadhi ya kaya Wilayani humo, ni kutokana na ukosefu wa maeneo ya kutosha kwa ajili ya shughuli za kilimo na uzalishaji. 

Kampeni hiyo iliyozinduliwa rasmi mapema Februari 11 Mwaka huu na Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi kupitia mradi wa urejeshaji hali kwa maeneo yaliyokumbwa na majanga Mkoani Kagera, unaotekelezwa chini ya Shirika la Chakula Duniani “FAO” Wilaya ya Misenyi ikiwa ni miongoni mwa Wilaya tano zenye wahanga, Imebainika kuwa ukiacha sababu za Tetemeko, Mvua, Magonjwa ya mimea na mazao, pia sababu nyingine ni ukosefu wa sehemu ya kutosha kufanya shughuli za Kilimo, Ufugaji na Uzalishaji kwa baadhi ya maeneo lengwa. 

Kijiji Nkerenge kilichopo Kata Mtukula Wilayani Misenyi ni miongoni mwa Vijiji vilivyolengwa kufikiwa na mradi huo, licha ya kubainika kuwa Kaya 68 kati ya 720 Zinazopatikana Eneo la Mkagando, hazina sehemu ya kutosha kufanya shughuli za kilimo kufuatia changamoto kubwa ya Uwepo wa Kitalu namba 19, kinachomilikiwa na NARCO. 

 Bwana Martin Adam (58) Mkazi wa Kijiji Nkerenge eneo la Mkagando, ni mhanga wa mgogoro huo wa Ardhi kati ya NARCO na wananchi hao ambae anasema kuwa awali kabla ya kitalu hicho walikuwa na mashamba ya kutosha kuweza kulima mazao mbalimbali, tofauti na sasa baada ya kuhamishwa maeneo yao na kupewa heka mbili mbili kwa kila kaya, hivyo mazao mengine ambayo walizoea kulima kama mazao ya mbogamboga, kwa sasa yamepotea kulingana na ardhi kuwa finyu. Hivyo Bwn Martin anapeleka kilio chake kwa Serikali kuwatenegea maeneo ya kutosha ili kuweza kuzinusuru kaya hizi nazo ziweze kukabiliana na Utapiamlo na magonjwa yanayoweza kuvikabili vizazi vyao kufuatia ukosefu wa lishe bora. 

Kwa mujibu wa ripoti ya Kaimu Mratibu wa mradi huo Ndg, Amoni Lugeiyamu, anasema kuwa Kampeni ya Mafunzo ya Lishe na Usindikaji wamelenga kuvifikia Vijiji vinne Wilayani humo ambavyo ni Nyankere, Nkerenge, Minziro na Kikono, huku ikiwa tayari mafunzo hayo yamekwishawafikia wanavikundi wa Vijiji vitatu vya Nkerenge, Nyankere na Minziro na yatahitimishwa katika kijiji cha kikono Kata Buyango Wilayani Misenyi. 

Vijiji hivi kupitia mradi wa urejeshaji hali unaofadhiliwa na FAO tayari vimegawiwa Mbegu (vipando), kuku na vifaranga vya Samaki, maharage yenye virutubisho aina ya Jesca, na sasa Kampeni hii inalenga kuwajengea uwezo wa kuzalisha na kusindika mazao yanayopatikana kupitia mavuno ya Vpando na Mbegu walizogawiwa awali. 

Kutokana na mazao hayo tayari Vikundi vimejengewa uwezo wa kutengeneza vyakula mbalimbali kwa ajili ya lishe bora, ikiwemo uji wa lishe, keki, andazi, supu ya maharage, uji wa unga wa maharage, pilau la maharage, pilau la viazi lishe na maharage n.k
 Pichani ni chungu cha pilau ya Viazi Lishe na Maharage kikiendelea kupikwa baada ya somo katika Kampeni ya Lishe na Usindikaji Mutukula.
Ndugu Amoni Lugeiyamu akitoa ufafanuzi kwa Vikundi vya Wakulima na wafugaji kuhusu Kampeni ya Mafunzo ya Lishe na Usindikaji, katika Kijiji cha Minziro Wilayani Misenyi
Martin Adamu Mkazi wa Mkagando Kijiji Nkerenge ni mmoja kati ya kaya 68 zilizoathiriwa na Kitalu namba 19, na kusababisha ukosefu wa Lishe Bora kwenye familia yake, kufuatia ufinyu wa ardhi kwa shughuli za Kilimo
Fredrick Kitone Mkulima na Msindikaji wa Vyakula akiendelea na somo la Mapishi ya keki itokanayo na Viazi Lishe, Wakati wa mafunzo ya Lishe na Usindikaji Mutukula Misenyi
 Pichani ni Bi Frola Paul Mkazi wa Minziro akimywesha uji mwanae Mara baada ya kupata mafunzo ya upikaji Lishe ya Uji wa Maharage ya Jesca.


Hivyo makala UKOSEFU WA MAENEO YA KILIMO UNACHANGIA LISHE DUNI MISENYI

yaani makala yote UKOSEFU WA MAENEO YA KILIMO UNACHANGIA LISHE DUNI MISENYI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UKOSEFU WA MAENEO YA KILIMO UNACHANGIA LISHE DUNI MISENYI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/ukosefu-wa-maeneo-ya-kilimo-unachangia.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "UKOSEFU WA MAENEO YA KILIMO UNACHANGIA LISHE DUNI MISENYI"

Post a Comment

Loading...