Loading...

Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu:Vyanzo maji visimamiwe kwa vizazi vya sasa na vijavyo

Loading...
Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu:Vyanzo maji visimamiwe kwa vizazi vya sasa na vijavyo - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu:Vyanzo maji visimamiwe kwa vizazi vya sasa na vijavyo, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu:Vyanzo maji visimamiwe kwa vizazi vya sasa na vijavyo
link : Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu:Vyanzo maji visimamiwe kwa vizazi vya sasa na vijavyo

soma pia


Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu:Vyanzo maji visimamiwe kwa vizazi vya sasa na vijavyo

 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu imesema kuwa vyanzo vya maji ni lazima visimamiwe kuhakikisha rasilimali hiyo ya maji inapatikana ya kutosha na inakuwa endelevu kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Huduma ya upatikanaji wa maji ambayo kupitia watoa huduma hiyo hususani mamlaka za maji, yanatokana na uhifadhi unaofanywa na Bodi za Maji za Mabonde (ambayo ni 9) yaliyopo nchini ambapo yanayotekeleza Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Na. 11 ya Mwaka 2009.

Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Maji ya Bonde Wami/Ruvu Hamza Sadiki wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Warsha Maalumu kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa Usimamizi na Utunzaji wa Rasilimali za Maji iliyoandaliwa na Bodi.

Amesema Bodi hiyo ndio wasimamizi wa vyanzo vyote vya maji vilivyopo kwenye Bonde la Wami/Ruvu ambalo linapita kwenye mikoa 7 ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma, Manyara, Tanga na…hivyo ni lazima wasambazaji wote wa maji hayo wapate kibali kutoka bonde hilo.

Akisisitiza kuwa wananchi wengi wana uelewa mdogo kuhusiana na uhifadhi wa maji na kusababisha vyanzo hivyo kuingiliwa na shughuli mbalimbali za kibidamu zikiwemo uvuvi, kilimo pamoja na ufugaji.

“Vyanzo vya maji nchini chanzo kikuu ni mvua, hivyo kila mmoja akivuna maji ya mvua. Mwisho wa siku maji hayo yanayohifadhiwa chini ya ardhi na kutumika kama vyanzo vya chini na juu ya ardhi yatakosekana”, amesema Mwenyekiti.
Mwakilishi wa Afisa wa Maji wa Bonde la Wami\Ruvu Mshuda Wilson amesema kuwa visima vinavyochimbwa vinatakiwa kuwa na kibali kuendelea kumiliki kisima hicho ni kosa la kisheria.

Sheria inakataa uchafuzi wa mazingira na inapotokea mtu anachafua maji ikiwemo utiririshaji maji maji katika vyanzo vya maji yatakiwa kuipimwa na ndipo yaweze kurudishwa katika vyanzo hivyo. Amesema shughuli za kibidamu katika ndani ya mita 60 ya vyanzo ya maji zinazuiliwa kufanyika na kuwepo shughuli hizo ni kinyume cha sheria ya maji ya usimamizi wa rasilimali za maji. 

Amesema kuwa maji ya mvua nayo uvunaji wake unaangaliwa kwa kiwango endapo kiwango kitazidi zaidi lita 20,000 lazima uvunaji wa maji hayo yapate kibali.
Mwenyekiti wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu Hamza Sadiki. Akizungumza na waandishi wa Habari wa akifungua warsha ya Bonde la Wami/Ruvu

 Mwakilishi wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu Mshuda Wilson akitoa taarifa Bonde la wami/Ruvu katika warsha ya waandishi habari kuhusiana na uhifadhi wa vyanzo vya maji


Hivyo makala Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu:Vyanzo maji visimamiwe kwa vizazi vya sasa na vijavyo

yaani makala yote Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu:Vyanzo maji visimamiwe kwa vizazi vya sasa na vijavyo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu:Vyanzo maji visimamiwe kwa vizazi vya sasa na vijavyo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/bodi-ya-bonde-la-wamiruvuvyanzo-maji.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu:Vyanzo maji visimamiwe kwa vizazi vya sasa na vijavyo"

Post a Comment

Loading...