Loading...
title : Diwani kata ya Lemara Profesa Raymond Mosha akabidhi baiskeli ya walemavu kwa mkazi wa kata hiyo George Makinda
link : Diwani kata ya Lemara Profesa Raymond Mosha akabidhi baiskeli ya walemavu kwa mkazi wa kata hiyo George Makinda
Diwani kata ya Lemara Profesa Raymond Mosha akabidhi baiskeli ya walemavu kwa mkazi wa kata hiyo George Makinda
Na Ahmed Mahmoud,Arusha.
Diwani wa Kata ya Lemara ,Profesa Raymond Mosha ameanzisha mpango wa kuwafikia watu wenye ulemavu na kuwapatia mahitaji yao pamoja na nyenzo wanazohitaji ikiwemo baiskeli maalumu za walemavu.
Akizungumza katika zoezi la kukabidhi baiskeli ya mlemavu mwenye umri wa miaka zaidia ya sitini mkazi anayeitwa Mzee George Makinda wa kata ya Lemara katika eneo la Njiro jijini Arusha amesema kuwa baiskeli hiyo itamsaidia kujishughulisha na kazi zake kama kawaida.
Msaada wa baiskeli hiyo imetolewa na Professa Raymond Mosha ambae ni diwani wa kata hiyo ya Lemara baada ya kuona familia ya Mzee George Makinda haina uwezo wa ununuzi wa baiskeli hiyo,
Professa Mosha alisema kuwa alihuzunishwa sana na maisha ya mlemavu huyo kwani George Makinda miaka ya nyuma alikua mzima lakini alikubwa na ugonjwa wa kupooza uliomfanya kua mlemavu wa kushindwa kuongea wala kutembea.
alisema hali hiyo ndio iliomgusa yeye na marafiki zake nakuamua kujitolea baiskel ambayo itamsaidia kwa namna moja au nyingine kutembelea na kujiona kama watu wengine.
Hata hivyo Mke wa Mzee George Makinda Bi Estar Makinda pamoja na kutoa shukurani ya msaada wa Baiskel hiyo ambayo anataja kua sababu ya kumfanya kumpa ahuweni kwakua ameteseka kwa muda mrefu katika kumlea mumewe,
Estar alisema hata muda mwingine alishindwa kujishughulisha na kazi za kiuchumi nakubaki kumhudumia mumewe kutokana na muda wote ni mtu wa kuhudumiwa kila kitu,
“ sasa amepatiwa msaada wa Baisekel itakayomsaidia kutembea naamini sasa mabadiliko ya familia yataonekana” Alisema Estar Makinda.
Diwani wa kata ya Lemara Profesa Raymond Mosha akikabidhi baiskeli ya walemavu kwa mkazi wa kata hiyo George Makinda ambaye ni mlemavu wa miguu baada ya kupata ugonjwa wa kupooza .picha zota na Mahmoud Ahmad Arusha
Hivyo makala Diwani kata ya Lemara Profesa Raymond Mosha akabidhi baiskeli ya walemavu kwa mkazi wa kata hiyo George Makinda
yaani makala yote Diwani kata ya Lemara Profesa Raymond Mosha akabidhi baiskeli ya walemavu kwa mkazi wa kata hiyo George Makinda Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Diwani kata ya Lemara Profesa Raymond Mosha akabidhi baiskeli ya walemavu kwa mkazi wa kata hiyo George Makinda mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/diwani-kata-ya-lemara-profesa-raymond.html
0 Response to "Diwani kata ya Lemara Profesa Raymond Mosha akabidhi baiskeli ya walemavu kwa mkazi wa kata hiyo George Makinda"
Post a Comment