Loading...

KAMATI YA BUNGE YATAKA MFUKO WA TAIFA WA UKIMWI KUJITEGEMEA

Loading...
KAMATI YA BUNGE YATAKA MFUKO WA TAIFA WA UKIMWI KUJITEGEMEA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KAMATI YA BUNGE YATAKA MFUKO WA TAIFA WA UKIMWI KUJITEGEMEA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KAMATI YA BUNGE YATAKA MFUKO WA TAIFA WA UKIMWI KUJITEGEMEA
link : KAMATI YA BUNGE YATAKA MFUKO WA TAIFA WA UKIMWI KUJITEGEMEA

soma pia


KAMATI YA BUNGE YATAKA MFUKO WA TAIFA WA UKIMWI KUJITEGEMEA



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akisema jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia Masuala ya UKIMWI na Madawa ya Kulevya mapema jana
Mama Salma Kikwete, Mjumbe wa Kamati ya Bunge inajishughulishana Masuala ya UKIMWI na Madawa ya Kulevya akisoma nyaraka wakati wa ziara ya kamati walipotembelea Shule ya Sekondari Makoka.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge inajishughulisha na Masuala ya UKIMWI na Madawa ya Kulevya Mama Salma Kikwete (kulia) akisalimiana na Suzana Paul mwanafunzi katika Shule ya Sekondari Makoka.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia Masuala ya UKIMWI na Madwa ya Kulevya, Mhe. Oscar Mukasa akisema jambo kwa wajumbe wa kamati hiyo (hawapo pichani) katika ziara ya wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea Mkoa wa Dar Es Salaam kujionea hali ya utoaji wa huduma za afya kwenye matibabu ya Virusi vya Ukimwi.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia Masuala ya UKIMWI na Madawa wakimsikiliza mtoa huduma za afya katika Kituo cha kutolea dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi (CTC) katika Hospitali ya Sinza.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia Masualaya UKIMWI na Madawa (waliosimama) wakimsikiliza mtoahudumazaafyakatikaKituo cha kutoleadawazakufubazaVirusivytaUkimwi (CTC) katikaHospitaliyaSinza



……………………..

Na WAMJW – Dar Es Salaam.

Serikali imetakiwa kutenga bajeti ya kutosheleza ili kuuwezesha Mfuko wa Taifa wa Ukimwi kujitegemea na kuepukana na utegemezi wa fedha za wafadhili katika mapambano ya Virusi vya Ukimwi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia masuala ya UKIMWI na Madawa ya kulevya Oscar Mukasa wakati wa kamati hiyo ilipofanya ziara katika Kitengo cha kutolea dawa za kufubaza Virusi vya UKIMWI (CTC) katika Hospitali ya Wilaya ya Ubungo kujionea hali ya utoaji huduma.

Mhe. Oscar Mukasa (MB) amesema suala la upatikanaji wa dawa za kufubaza virusi vya ukimwi ni jambo la kitaifa na kamati yake ina mkakati wa kuhakikisha inaongeza nguvu kwenye Mfuko wa Taifa wa Ukimwi (ATF) na nchi kuweza kujitegemea kuhusu masuala ya UKIMWI.

“Tuna haja ya kujipanga wenyewe kuhakikisha kwamba tunajitegemea, ule utegemezi wa fedha za wadau za mapambano ya Ukimwi unaweza kupungua”. amesema Mhe. Mukasa. Mhe. Mukasa amesema Serikali imekuwa ikitegemea fedha za wafadhili kutoka nje ya nchi na sasa ni vizuri tukajipanga wenyewe na kuacha utegemezi wa wafadhili hao kutoa fedha muda wote.

Hata hivyo Mhe. Mukasa amesema kamati yake itaendelea kusimamia Serikali hasa Wizara ya fedha na Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha wanapata chanzo mahsusi cha kodi kwa ajili ya ATF.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati hiyo na pia Waziri mwenye dhamana ya Afya, Maendeleo ye Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu amefurahishwa kuona Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeanza kutekeleza agizo alilolitoa la kutoa ushauri, kupima pamoja na matibabu ya kufubaza virusi vya ukimwi.

Aidha, Waziri Ummy ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kutekeleza agizo la Serikali kwa kutoa dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi kwa muda kwa kipindi cha miezi mitatu kwa wagonjwa ambao wameshachunguzwa na kubainika virusi kufubaa.

“Mpango wetu Serikali kwa wagonjwa ambao watakao kidhi vigezo basi watazipate dawa hizo kwa miezi sita”. Alisema Waziri Ummy na kuendelea kuwa wanalenga kuwaondolea usumbufu wa kuja mara kwa mara


Hivyo makala KAMATI YA BUNGE YATAKA MFUKO WA TAIFA WA UKIMWI KUJITEGEMEA

yaani makala yote KAMATI YA BUNGE YATAKA MFUKO WA TAIFA WA UKIMWI KUJITEGEMEA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KAMATI YA BUNGE YATAKA MFUKO WA TAIFA WA UKIMWI KUJITEGEMEA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/kamati-ya-bunge-yataka-mfuko-wa-taifa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "KAMATI YA BUNGE YATAKA MFUKO WA TAIFA WA UKIMWI KUJITEGEMEA"

Post a Comment

Loading...