Loading...
title : PRESHA YA MO YA DAKIKA TATU ZA MWISHO ZA MCHEZO WA SIMBA NA AS VITA ZILIVYOGEUKA FURAHA ILIYOPITILIZA
link : PRESHA YA MO YA DAKIKA TATU ZA MWISHO ZA MCHEZO WA SIMBA NA AS VITA ZILIVYOGEUKA FURAHA ILIYOPITILIZA
PRESHA YA MO YA DAKIKA TATU ZA MWISHO ZA MCHEZO WA SIMBA NA AS VITA ZILIVYOGEUKA FURAHA ILIYOPITILIZA
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Mwekezaji wa Klabu ya Soka ya Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ kwa mara ya kwanza ameonyesha hisia zake na mapenzi kwa klabu hiyo katika mchezo wa mwisho wa Kundi D la Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita Club ya DR Congo, ambapo Simba SC iliondoka na ushindi wa bao 2-1 na kufuzu Robo Fainali ya Michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa ngazi ya klabu.
Katika mchezo huo uliopigwa dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam majira ya Saa 1 Usiku, Simba SC ilionyesha kiwango bora na kupata ushindi huo mbele ya timu ngumu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Vita Club.
Mohammed Dewji ‘MO’ akiwa na furaha iliyoje! siku hiyo baada ya ushindi huo wa Simba SC, MO ametuma picha yenye ujumbe iliyojawa na hisia ya huzuni na masikitiko kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Instagram wakati huo kabla pambano kumalizika.
Ujumbe huo umeandikwa hivi: ‘’Hizi Picha zilipigwa zikiwa zimebaki dakika 3 kabla ya mpira kuisha. Tulikuwa na wasiwasi, Pressure ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba vidole vilikuwa na ganzi. Somo: Usikate tama. Mipango ya Mungu haina makosa! AMEEN’’
Baada ya matokeo hayo, Simba SC imetinga hatua ya Robo Fainali ya Michuano hiyo, hata hivyo itasubiri March 20 droo ya Robo Fainali itakayofanyika nchini Misri.
Hivyo makala PRESHA YA MO YA DAKIKA TATU ZA MWISHO ZA MCHEZO WA SIMBA NA AS VITA ZILIVYOGEUKA FURAHA ILIYOPITILIZA
yaani makala yote PRESHA YA MO YA DAKIKA TATU ZA MWISHO ZA MCHEZO WA SIMBA NA AS VITA ZILIVYOGEUKA FURAHA ILIYOPITILIZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PRESHA YA MO YA DAKIKA TATU ZA MWISHO ZA MCHEZO WA SIMBA NA AS VITA ZILIVYOGEUKA FURAHA ILIYOPITILIZA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/presha-ya-mo-ya-dakika-tatu-za-mwisho.html
0 Response to "PRESHA YA MO YA DAKIKA TATU ZA MWISHO ZA MCHEZO WA SIMBA NA AS VITA ZILIVYOGEUKA FURAHA ILIYOPITILIZA"
Post a Comment