Loading...
title : TUNDURU WAFANIKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOKUWEPO KATIKA SHULE ZA SEKONDARI
link : TUNDURU WAFANIKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOKUWEPO KATIKA SHULE ZA SEKONDARI
TUNDURU WAFANIKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOKUWEPO KATIKA SHULE ZA SEKONDARI
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
WILAYA ya Tunduru imefanikiwa kumaliza changamoto mbalimbali kwa baadhi ya shule za sekondari wilayani humo ikiwemo ya ukosefu wa vitanda katika Shule ya Sekondari Namasakata .
Kutatuliwa kwa changamoto hiyo kunatokana na jitihada mbalimbali ambazo zimewekwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera kwa kushirikiana na timu ya wataalam wa Wilaya na wananchi.
Akizungumza na Michuzi Blog jana Machi 10,2019 ,Mkuu wa Wilaya hiyo Homera amesema kuwa katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo wametumia fursa ya uwepo wa mfuko wa elimu kutokana na mazao mbalimbali yanayolimwa wilayani hapo.
Amefafanua kuwa wadau wa zao la ufuta waliridhia kukatwa mkulima sh.30 kwa kila kilo na kufanikiwa kukusanya zaidi ya Sh.milioni 27 ambazo zimetumika kutengeneza miundombinu kama vile kujenga vyoo vya walimu Namwinyu sekondari, na kutengeneza vitanda 58 (double deka).
Pia ujenzi wa vyoo katika shule ya sekondari Namasakata na kufanikiwa kuwapatia vitanda wanafunzi 116 kwa wakati mmoja. Aidha Homera amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Tunduru Gasper Balyomi kwa usimamizi thabiti wa fedha zinazochangwa na wananchi kupitia mazao yao na harambee mbalimbali.
Hata hivyo Homera na timu yake wamefanikiwa kukusanya zaidi ya Sh. milion 60 katika harambee ya kuchangia ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari ambazo na Serikali kuu kuunga mkono nguvu za wananchi kwa kuiletea Sh.milion 137.5 ili kukamilisha madarasa hayo na samani zake.
"Tunawashukuru wadau wa maendeleo,wananchi wa Tunduru kutokana na kila aina ya ushirikiano ambao wanautoa kuhakikisha tunaondoa changamoto katika sekta ya elimu. Meza na viti).#Tukutane site ,Tukutane Kazini#," amesema Homera.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera akizungumza jambo kwenye moja ya kikao cha kuhakikisha kinafanikiwa kumaliza changamoto mbalimbali kwa baadhi ya shule za sekondari wilayani humo ikiwemo ya ukosefu wa vitanda katika Shule ya Sekondari Namasakata .
Hivyo makala TUNDURU WAFANIKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOKUWEPO KATIKA SHULE ZA SEKONDARI
yaani makala yote TUNDURU WAFANIKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOKUWEPO KATIKA SHULE ZA SEKONDARI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TUNDURU WAFANIKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOKUWEPO KATIKA SHULE ZA SEKONDARI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/tunduru-wafanikiwa-kutatua-changamoto.html
0 Response to "TUNDURU WAFANIKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOKUWEPO KATIKA SHULE ZA SEKONDARI"
Post a Comment