Loading...
title : Ateuliwa kuongoza Shirika la Viwango
link : Ateuliwa kuongoza Shirika la Viwango
Ateuliwa kuongoza Shirika la Viwango
Suleiman Msuya
Profesa Egid Mubofu |
RAIS John Magufuli amemteua Profesa Egid Mubofu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Joseph Masikitiko.
Taarifa ya Ikulu iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi ilionesha kuwa uteuzi huo ulianza jana.
Profesa Mubofu alikuwa akikaimu nafasi hiyo kwa muda sasa, hivyo Rais kumwidhinisha moja kwa moja kuongoza TBS ambayo ni taasisi muhimu kwa nchi.
Kabla ya Mubofu kuteuliwa kukaimu nafasi hiyo, alikuwa Mkuu wa Idara ya Kemia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Masikitiko ni mmoja wa wakurugenzi ambao walitumbuliwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.
Katika kadhia hiyo, Mwijage alimsimamisha pia Meneja wa Fedha, Mipango na Utawala wa TBS, Emmanuel Ntelya pia kupisha uchunguzi.
Hivyo makala Ateuliwa kuongoza Shirika la Viwango
yaani makala yote Ateuliwa kuongoza Shirika la Viwango Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Ateuliwa kuongoza Shirika la Viwango mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/ateuliwa-kuongoza-shirika-la-viwango.html
0 Response to "Ateuliwa kuongoza Shirika la Viwango"
Post a Comment