Loading...
title : Makada wa CCM vyuo vikuu wapewa vyeti
link : Makada wa CCM vyuo vikuu wapewa vyeti
Makada wa CCM vyuo vikuu wapewa vyeti
Mwandishi Wetu
Humphrey Polepole |
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, amekabidhi vyeti 402 kwa wanachama wa CCM wanaotarajia kuhitimu elimu ya juu katika vyuo vikuu vya mkoa wa Dodoma.
Polepole alikabidhi vyeti hivyo katika ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM makao makuu ambako viongozi mbalimbali wa chama na Serikali walihudhuria.
Akizungumza na wahitimu hao, Polepole aliwataka kuwa mfano mwema katika jamii kwani hiyo ndio sifa ya mwana CCM.
Aidha aliwasisitiza wale wenye sifa na vigezo wasisite kuomba nafasi ndani ya CCM katika wakati huu ambao CCM ipo kwenye uchaguzi wa ngazi zote na jumuiya zote.
“Nawahakikishia CCM mpya hakuna mtu atakayehujumiwa akiomba uongozi kinachotakiwa ni kuzingatia maadali,” alisema.
Alisema CCM inajali makundi yote, hivyo kila mwanachama ana haki ya kugombea bila kuhofia mwingine ila kinachotakiwa ni kufuata taratibu ili kutochafua chama.
Kwa upande wake, Katibu wa Idara ya Vyuo Vikuu, Daniel Zenda alisema wao wamejipanga kujenga vijana wa vyuo mbalimbali kukiamini na kujenga chama jambo ambao limeanza kutumia.
Zenda alisema vijana katika vyuo vingi nchini wameonesha kuwa na imani na Serikali ya Awamu ya Tano, hivyo akaiomba CCM kuwapa ushirikiano ili kukidhi malengo yao.
Alisema katika vyuo wapo wanafunzi wengi ambao ni wana CCM ila hawapendi kujionesha moja kwa moja ili kuepusha migongano.
Hivyo makala Makada wa CCM vyuo vikuu wapewa vyeti
yaani makala yote Makada wa CCM vyuo vikuu wapewa vyeti Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Makada wa CCM vyuo vikuu wapewa vyeti mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/makada-wa-ccm-vyuo-vikuu-wapewa-vyeti.html
0 Response to "Makada wa CCM vyuo vikuu wapewa vyeti"
Post a Comment