Loading...
title : ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI KWA WITO WA KUIMARISHWA HUDUMA ZA UZAZI KATIKA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA VIJIJINI
link : ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI KWA WITO WA KUIMARISHWA HUDUMA ZA UZAZI KATIKA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA VIJIJINI
ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI KWA WITO WA KUIMARISHWA HUDUMA ZA UZAZI KATIKA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA VIJIJINI
Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar.
Hospitali na Vituo vya Afya vya Wilaya vinaweza kupunguza idadi ya akinamama kujifungulia Hospitali kuu ya Mnazimmoja iwapo juhudi za kuandaa mazingira mazuri zitachukuliwa na wakunga na wauguzi wa vituo hivyo.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo ameeleza hayo katika maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Wasanii Rahaleo.
Amesema akinamama wengi wamejenga imani ya kujifungua Hospitali kuu ya Mnazimmoja na kupelekea upungufu wa nafasi katika Hospitali hiyo huku vituo vya Afya vijijini vikiwa na akina mama wacheche wanaokwenda kwa huduma ya kuzaa.
Ameongeza kuwa Hospitali ya Mnazimmoja inazalisha zaidi ya akinamama 50 kwa siku na Mwembeladu wanawake 30 wengi wao kutoka vijijini wakati vituo vya afya vya huko vinazallisha wanawake wawili hadi watano kwa siku.
Waziri Mahmoud amewataka wakunga na wauguzi wa vituo vya afya vya Wilaya vinavyotoa huduma ya kuzalisha kuandaa mazingira yatakayowavutia wanawake kujifungua katika vituo vyao.
Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea na mkakati wa kuandaa mazingira mazuri na kuweka miundo mbinu bora ikiwemo vifaa vya kisasa hivyo amewataka wafanyakazi nao kubadilika na kuwapa faraja wagonjwa ili wajenge imani kwao.
Brass band ya Chipikizi ikiongoza maandamano ya wakunga na wauguzi kupita mbele ya mgeni rasmi Waziri Afya Mhmoud Thabit Kombo katika maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Wasanii Rahaleo Mjini Zanzibar.
Mama Mariyam Othmani Mihale akiongoza wakunga na wauguzi katika wimbo maalum wa maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani katika ukumbi wa Wasanii Rahaleo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wuguzi na Wakunga Zanzibar Amina Abdulkadir Ali akitoa maelezo juu ya siku ya Wuguzi duniani katika maadhimisho yaliyofanyika ukumbi wa wasanii Rahaleo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI KWA WITO WA KUIMARISHWA HUDUMA ZA UZAZI KATIKA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA VIJIJINI
yaani makala yote ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI KWA WITO WA KUIMARISHWA HUDUMA ZA UZAZI KATIKA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA VIJIJINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI KWA WITO WA KUIMARISHWA HUDUMA ZA UZAZI KATIKA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA VIJIJINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/zanzibar-yaadhimisha-siku-ya-wauguzi.html
0 Response to "ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI KWA WITO WA KUIMARISHWA HUDUMA ZA UZAZI KATIKA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA VIJIJINI"
Post a Comment