Loading...
title : MKUTANO WA KITAIFA WA WADAU WA ELIMU NA CHAMA CHA WALIMU WAFANYIKA JIJINI DAR
link : MKUTANO WA KITAIFA WA WADAU WA ELIMU NA CHAMA CHA WALIMU WAFANYIKA JIJINI DAR
MKUTANO WA KITAIFA WA WADAU WA ELIMU NA CHAMA CHA WALIMU WAFANYIKA JIJINI DAR
Shirika la ActionAid-Tanzania, Mtandao wa Elimu Tanzania, Shirika la Maendeleo ya Elimu Singida-MEDO na Mtandao wa Asasi za Kiraia-KINGONET kwa pamoja wanatekeleza mradi wa uhamasishaji utoaji elimu bora kupitia rasilmali zetu wenyewe ( PROMOTING QUALITY EDUCATION THROUGH PROGRESSIVE DOMESTIC RESOURCE MOBILIZATION) unaotekelezwa huko Kilwa na Singida Vijijini kwa ngazi ya wilaya kwa kufanya kazi na kamati za shule na klabu za haki za watoto shuleni.
Kitaifa MRADI Huo unalenga kufanya utetezi wa mabadiliko ya kisera na sheria hasa suala la ulipaji kodi, ukusanyaji kodi kwa haki (tax Justice), uzibaji wa mianya ya uvujaji wa kodi ili makusanyo yaongezeke na yagharimie huduma bora kwa wananchi wa Tanzania hususani kuboresha utoaji wa Elimu bora Nchini.
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania Bi. Cathleen Sekwao akifungua mkutano huo aligusia pia kuhusu “utoaji wa huduma za jamii hapa nchini unakabiliwa na ufinyu wa fedha, wote tu mashahidi kuwa hadi kufikia mwezi Machi, 2017 serikali ilikuwa imetoa asilimia 34 tu ya bajeti yote ya 2016/2017.
Jambo hili lina madhara makubwa katika utoaji wa huduma za jamii hasa elimu msingi yenye ubora hasakwa mtoto wa kike”.
Jambo hili lina madhara makubwa katika utoaji wa huduma za jamii hasa elimu msingi yenye ubora hasakwa mtoto wa kike”.
Aliongelea pia serikali kushindwa kutoa asilimia mia moja ya fedha za kutekeleza bajeti ya 2016/2017 tafiti zinaonyesha kuwa Tanzania inapoteza fedha nyingi kupitia misamaha ya kodi.
Mwakilishi kutoka Mtandao wa Kodi Tanzania (TTJC), Grace Masalakulangwa akiwasilisha ripoti ya utafiti ya One Billion Question iliyotafitiwa na shirika la ISCEJIE katika Mkutano uliowakutanisha wadau wa Elimu na Wenyeviti wa Chama cha Walimu ngazi ya mikoa ya Tanzania Bara iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Afisa Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Alistidia Kamugisha akifungua mkutano na kuwaelezea malengo ya mkutano huo wa siku mbili kwa wadau wa elimu na Chama cha Walimu Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET), Cathleen Sekwao akitoa mada kuhusu umuhimu wa ukusanyaji wa rasilimali za ndani na kuwekeza katika kuboresha sekta ya elimu hususani kwa mtoto wa kike na maslahi ya walimu katika mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU).
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MKUTANO WA KITAIFA WA WADAU WA ELIMU NA CHAMA CHA WALIMU WAFANYIKA JIJINI DAR
yaani makala yote MKUTANO WA KITAIFA WA WADAU WA ELIMU NA CHAMA CHA WALIMU WAFANYIKA JIJINI DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKUTANO WA KITAIFA WA WADAU WA ELIMU NA CHAMA CHA WALIMU WAFANYIKA JIJINI DAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/mkutano-wa-kitaifa-wa-wadau-wa-elimu-na.html
0 Response to "MKUTANO WA KITAIFA WA WADAU WA ELIMU NA CHAMA CHA WALIMU WAFANYIKA JIJINI DAR"
Post a Comment