Loading...

RAIS MAGUFULI NI MZALENDO NAMBA MOJA –DK BANA

Loading...
RAIS MAGUFULI NI MZALENDO NAMBA MOJA –DK BANA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RAIS MAGUFULI NI MZALENDO NAMBA MOJA –DK BANA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RAIS MAGUFULI NI MZALENDO NAMBA MOJA –DK BANA
link : RAIS MAGUFULI NI MZALENDO NAMBA MOJA –DK BANA

soma pia


RAIS MAGUFULI NI MZALENDO NAMBA MOJA –DK BANA

Jovina Bujulu-MAELEZO.

Baadhi ya wasomi wameonyesha kuridhishwa na kuunga mkono hatua ya Rais John Magufuli kuagiza wahusika wote wachukuliwe hatua za kisheria baada ya kupokea ripoti ya pili ya Kamati ya Wachumi na Wanasheria aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza Mchanga wa Madini unaosafirishwa kwenda nje ya nchi.

Akiongea na Idara ya Habari (Maelezo) Dk Benson Bana ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema kitendo kilichofanywa na Rais Magufuli kimewafungua macho viongozi wengi wa Afrika na dunia na kitakuwa ni mfano wa kuigwa kwa Serikali nyingi za Afrika na dunia kwa ujumla

“Ningefurahi kama tungetenga siku maalumu kuandamana kwa nia ya kuunga mkono nia njema ya Rais ya kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi hii hazitumiwi hovyo hovyo” amesema Dk Bana.

Aliongeza kusema kuwa kitendo cha kutafuta ukweli katika makinikia na biashara ya madini na kuweka wazi taarifa hiyo kwa umma  na kusema wahusika wa sakata hilo wachukuliwe hatua za kisheria kimeonyesha uzalendo wa dhati kwa nchi yake.

Aidha aliunga mkono kitendo cha Rais kukubali kufanyia kazi mapendekezo yote 21 yaliyotolewa na Tume ya Uchunguzi, kwani yataweka wazi mwenendo mzima wa biashara ya madini na kuziba mianya ya wizi wa madini.

Dk. Bana alimpongeza pia Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba kwa kuchukua uamuzi wa haraka wa kuwazuia kusafiri nje ya nchi watuhumiwa wa sakata hilo.

Alisema wale wote waliotajwa kuhusika na suala hilo kukaa nje ya utumishi wa umma kwa muda wakati uchunguzi dhidi yao ukiendelea na  endapo watabainika kuwa hawana hatia warudishwe kazini na ikibainika kuwa walihusika wachukuliwe hatua stahiki.

Alitoa wito kwa Watanzania kuuunga mkono  nia njema ya Rais Magufuli kwa sababu hatua hiyo ni harakati za kuweka sawa uchumi wa nchi ili kuboresha maisha ya Watanzania.


Dkt. Benson Bana-Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 


Hivyo makala RAIS MAGUFULI NI MZALENDO NAMBA MOJA –DK BANA

yaani makala yote RAIS MAGUFULI NI MZALENDO NAMBA MOJA –DK BANA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RAIS MAGUFULI NI MZALENDO NAMBA MOJA –DK BANA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/rais-magufuli-ni-mzalendo-namba-moja-dk.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "RAIS MAGUFULI NI MZALENDO NAMBA MOJA –DK BANA"

Post a Comment

Loading...