Loading...

Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Awamu ya Pili Kufanyika Mwezi Agosti 2017

Loading...
Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Awamu ya Pili Kufanyika Mwezi Agosti 2017 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Awamu ya Pili Kufanyika Mwezi Agosti 2017, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Awamu ya Pili Kufanyika Mwezi Agosti 2017
link : Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Awamu ya Pili Kufanyika Mwezi Agosti 2017

soma pia


Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Awamu ya Pili Kufanyika Mwezi Agosti 2017


Na: Veronica Kazimoto
Dodoma
18 Julai, 2017.
Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania wa awamu ya pili unatarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya wadadisi yanayoendelea kufanyika mkoani Dodoma Meneja wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Wilfred Mwingira amesema  lengo kuu la utafiti huo ni kufuatilia viashiria vilivyowekwa kwenye utafiti wa awamu ya kwanza ili kutathmini na kujua kama kuna athari yoyote iliyotokea.

"Utafiti huu ni wa kitaifa na utafanyika Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la kutathmini na kujua kama kuna athari yoyote iliyojitokeza kwenye viashiria vilivyowekwa kwenye utafiti wa awamu ya kwanza", amesema Mwingira.

Nae Mratibu wa utafiti huo Rainer Kiama amesema kuwa utafiti huu unafanyika ili kutathmini kama mpango unaleta manufaa yaliyokusudiwa katika ngazi ya kaya kwa kutumia viashiria kama vile elimu, afya, kazi na matumizi ya muda, shughuli za kaya zisizo za kilimo, mapato, mikopo, akiba na uhamishaji fedha.

Viashiria vingine ni  shughuli za kilimo,  makazi ya kaya na upatikanaji wa maji, matumizi na usalama wa chakula katika  kaya, maamuzi katika kaya, ukatili kwa wanawake na matarajio ya vijana, mahusiano ya kaya na jamii pamoja na mtazamo wa kaya kuhusu Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania wa awamu ya pili utahusisha kaya takribani elfu saba (7,000)  ambazo zilihojiwa katika utafiti wa awamu wa kwanza uliofanyika mwezi Juni, 2015.


Hivyo makala Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Awamu ya Pili Kufanyika Mwezi Agosti 2017

yaani makala yote Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Awamu ya Pili Kufanyika Mwezi Agosti 2017 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Awamu ya Pili Kufanyika Mwezi Agosti 2017 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/utafiti-wa-mpango-wa-kunusuru-kaya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Awamu ya Pili Kufanyika Mwezi Agosti 2017"

Post a Comment

Loading...