Loading...
title : MBUNGE RITTA KABATI APOKEA KERO ZA WENYEVITI WA MITAA 192 YA MANISPAA YA IRINGA
link : MBUNGE RITTA KABATI APOKEA KERO ZA WENYEVITI WA MITAA 192 YA MANISPAA YA IRINGA
MBUNGE RITTA KABATI APOKEA KERO ZA WENYEVITI WA MITAA 192 YA MANISPAA YA IRINGA
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Wenyeviti wa mitaa 192 katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa wamelalamikia ufinyu wa posho wanayopata ukilinganisha na kazi wanazozifanya kuwatumikia wananchi kwa kuleta maendeleo.
Wakizungumza wakati wa mkutano mbunge wa viti maalumu mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wa kutoa kero zao na changamoto zinazowakabiri katika uwajibikaji wa majukumu yao huko mitaani.Wevyeviti hao walisema kuwa wamekuwa wakicheleweshewa posho zao toafauti na viongozi wengine na kuwasababisha kutofanya kazi kwa weledi wao unaotakiwa kwa kufikisha huduma stahiki.
Lakini wenyeviti hao walisema kuwa viongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa wamekuwa kero kwao kwa kutowasaidia kutatua changamoto na migogoro zilizopo kwenye mitaa hao.
"Huku mitaani watoto wadogo wanabakwa hovyo ukipeleka kesi polisi wanadai ushaidi haujakamilika na watuhumiwa wanakuwa nje kwa dhamana kitu kinachosababisha kudhohofisha utendaji wa kazi zao,mitaani kwenu kunawizi unaendelea lakini bado viongozi wa polisi wamekuwa kero kwa kutotatua kero hizo na swala jingine ni wenyeviti kudharauliwa na watumishi wa manispaa ya Iringa "walisema wenyeviti
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akizungumza na wenyeviti wa mitaa yote ya manispaa ya Iringa wakati wa kusikiliza kero zinazowakabili viongozi hao wakati wa utendaji wao huko wenye mitaa yao.
Hawa ni baadhi ya wenyeviti wa mitaa ya halmashauri ya manispaa ya Iringa waliohudhuria mkutano huo wa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta kabati
Hivyo makala MBUNGE RITTA KABATI APOKEA KERO ZA WENYEVITI WA MITAA 192 YA MANISPAA YA IRINGA
yaani makala yote MBUNGE RITTA KABATI APOKEA KERO ZA WENYEVITI WA MITAA 192 YA MANISPAA YA IRINGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MBUNGE RITTA KABATI APOKEA KERO ZA WENYEVITI WA MITAA 192 YA MANISPAA YA IRINGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/mbunge-ritta-kabati-apokea-kero-za.html
0 Response to "MBUNGE RITTA KABATI APOKEA KERO ZA WENYEVITI WA MITAA 192 YA MANISPAA YA IRINGA"
Post a Comment