Loading...
title : RC MAKONDA AZINDUA UJENZI WA OFISI ZA WALIMU DAR, KAZI YA UFYATUAJI TOTALI YA ANZA RASMI
link : RC MAKONDA AZINDUA UJENZI WA OFISI ZA WALIMU DAR, KAZI YA UFYATUAJI TOTALI YA ANZA RASMI
RC MAKONDA AZINDUA UJENZI WA OFISI ZA WALIMU DAR, KAZI YA UFYATUAJI TOTALI YA ANZA RASMI
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda aliye vaa fulani nye usi kulia akibebamatofali na askari wa Magereza na JKT, katika uzinduzi wa kuanza kupiga tofali za ujenzi wa ofisi za Walimu mkoa wa Dar es Salaam.
Mwambawahabari
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amezindua rasmi zoezi la Ufyatuaji wa Matofali kwaajili ya ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Walimu ambapo amewasihi Wadau na Wananchi kuunga Mkono jitiada hizo.
Katika uzinduzi huo RC Makonda ameshiriki zoezi la Ufyatuaji wa Matofali kwaajili ya Ujenzi huo.
Makonda amesema lengo la Ujenzi wa Ofisi hizo ni kuboresha Mazingira ya kufanya kazi kwa walimu ili waweze kutoa Elimu bora kwa Wanafunzi na kuongeza ufaulu.
Amesema wapo wengi waliopanga kufanya ujenzi wa Ofisi za Walimu lakini mipango hiyo iliishia kubaki kwenye makarabrasha maofisini lakini kupitia juhudi zake na Kamati aliyoiunda wameweza kuleta matokeo chanya.
RC Makonda ametoa wito kwa Wananchi na Wadau kuchangia Mabati, Saruji, Kokoto,Mchanga, Nondo au Nguvu kazi ilikuwawezesha walimu kufanyakazi katika mazingira bora.
Amesema ataki kuona kwenye Mkoa wake Walimu wanadhalilika kwa kukosa Ofisi na Vyoo hali inayopelekea kujisaidia kwa Majirani,Bar au Vichakani.
Aidha amesema hadi sasa amefanikiwa kupata mifuko zaidi ya 10,000 ya Saruji Mashine za kufyatulia Matofali,Gurdoza na vifaa vingine ambapo ataendelea kugonga hodi kwa Wadau ili waweze kuchangia ujenzi huo.
Amewaomba Wananchi kuwa na uzalendo kwa kujitoa katika ujenzi huo iwe kwa mtu binafsi au Vikundi vya Joaging,Timu za Mpira na vikundi vya maendeleo.
Ameipongeza Kamati ya ujenzi wa Ofisi za walimu,JKT,Jeshi la Magereza, Jeshi la Polisi,NHC, TBA,Channel Ten na Umoja wa Wamiliki wa Malori na wengine kwa namna wanavyojitoa kusaidia katika zoezi hilo.
Katika hatua nyingine RC Makonda amesema atatoa TV 30 kwa Magereza ya Ukonga, Segerea na Keko ili wafungwa wapate fursa za kutazama hotuba za Rais DR.JOHN MAGUFULI ili wajue maendeleo yanayofanyika uraiani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu Canal Charles Mbuge amesema hadi sasa kiasi cha fedha kilichotumika ni zaidi ya Million 200 ambapo watahakikisha ujenzi huo unakamilika.
Hivyo makala RC MAKONDA AZINDUA UJENZI WA OFISI ZA WALIMU DAR, KAZI YA UFYATUAJI TOTALI YA ANZA RASMI
yaani makala yote RC MAKONDA AZINDUA UJENZI WA OFISI ZA WALIMU DAR, KAZI YA UFYATUAJI TOTALI YA ANZA RASMI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MAKONDA AZINDUA UJENZI WA OFISI ZA WALIMU DAR, KAZI YA UFYATUAJI TOTALI YA ANZA RASMI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/rc-makonda-azindua-ujenzi-wa-ofisi-za.html
0 Response to "RC MAKONDA AZINDUA UJENZI WA OFISI ZA WALIMU DAR, KAZI YA UFYATUAJI TOTALI YA ANZA RASMI"
Post a Comment