Loading...

SERIKALI YATOA HATI MPYA ZA ARDHI DODOMA.

Loading...
SERIKALI YATOA HATI MPYA ZA ARDHI DODOMA. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YATOA HATI MPYA ZA ARDHI DODOMA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YATOA HATI MPYA ZA ARDHI DODOMA.
link : SERIKALI YATOA HATI MPYA ZA ARDHI DODOMA.

soma pia


SERIKALI YATOA HATI MPYA ZA ARDHI DODOMA.

Mwambawahabari
Serikali kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  imeanza kutoa hati mpya za ardhi zenye umri wa miaka 99 tofauti na zile zilizokuwa zikitolewa awali za miaka 33. 

Akizungumza na wanahabari leo Mjini Dodoma Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema  zoezi hilo la ubadilishaji wa hati kwa wakazi elfu 25 wa mkoa huo limeanza rasmi ambapo wakazi hao wanatakiwa kufika Wizarani wakiwa na nakala za hati zao za zamani ambazo zimelipiwa kodi zote za ardhi. 

“Ubadilishaji wa hati hizi ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipoivunja Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) ambapo aliiagiza Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kubadilisha hati zilizokuwa zikitolewa na mamlaka hiyo kutoka umiliki wa miaka 33 na kuwa miaka 99,” amefafanua Lukuvi. 

Ameongeza kuwa hati hizo za miaka 33 zilikuwa zikiwanyima fursa wakazi wa Dodoma kupata wawekezaji kutoka nje ya nchi kutokana na hati hizo  kuwa za muda mfupi tofauti na hati zinazotolewa na miji mingine hapa nchini. 

Aidha hati hizo pia zilikuwa kikwazo kwa wamiliki kushindwa kupata mikopo mikubwa ambayo hutolewa kwa watu wenye umiliki wa ardhi wa kuanzia miaka 50 na kuendelea. 

Lukuvi amesema kuwa mabadiliko hayo ya hati hayata athiri mipaka ya viwanja vitakavyobadilishiwa hati bali kinachofanyika ni kubadilisha umri wa umiliki wa ardhi.


Hivyo makala SERIKALI YATOA HATI MPYA ZA ARDHI DODOMA.

yaani makala yote SERIKALI YATOA HATI MPYA ZA ARDHI DODOMA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YATOA HATI MPYA ZA ARDHI DODOMA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/serikali-yatoa-hati-mpya-za-ardhi-dodoma.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI YATOA HATI MPYA ZA ARDHI DODOMA."

Post a Comment

Loading...