Loading...

TANZANIA IPO SALAMA NA IMARA -WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

Loading...
TANZANIA IPO SALAMA NA IMARA -WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TANZANIA IPO SALAMA NA IMARA -WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TANZANIA IPO SALAMA NA IMARA -WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA
link : TANZANIA IPO SALAMA NA IMARA -WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

soma pia


TANZANIA IPO SALAMA NA IMARA -WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania ipo salama na imara na kwamba mtu yeyote atakayejaribu kutaka kuvuruga amani atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Septemba 13, 2017) alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Bw. Mousa Farhang jijini Dar es Salaam.

“Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote kutoka popote atakayejaribu kuvuruga amani yetu. Nawaomba wananchi muwe makini na muendelee kuidumisha amani yetu.”Amesema kwa sasa Serikali ipo katika mapambano dhidi ya vitendo vya ufisadi, rushwa, biashara haramu ya dawa za kulevya pamoja na wahujumu uchumi.

Waziri Mkuu amesema licha ya Tanzania kuwa ni nchi ya amani na yenye utulivu wa kisiasa, wameendelea kuwahamasisha wananchi wake kudumisha mshikamano.Amesema mbali ya kuimarisha amani nchini, pia Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji jambo ambalo litawawezesha watakaokuja kuwekeza nchini kupata tija.

Hivyo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka nchini Iran ili waje kuwekeza kwenye viwanda mbalimbali vikiwemo vya kuchakata mazao ya kilimo.Pia amewakaribisha raia wa Iran kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyoko nchini Tanzania kama mlima wa Kilimanjaro, fukwe, mali kale na mbuga za wanyama.

Kwa upande wake, Balozi Farhang ameipongeza Serikali kwa kuwa na dhamira ya dhati ya kuimarisha uchumi na kupambana na dawa za kulevya na ufisadi.Balozi huyo amesema Serikali ya Irani ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi pamoja na vitendo vingine vya kihalifu.

Balozi Farhang ametumia fursa hiyo kuiomba Serikali ya Tanzania ifungue Ofisi ya Ubalozi nchini Iran ili kuimarisha uhusiano huo, ambapo Waziri Mkuu amekubali.Pia Bw. Farhang amesema aliwahi kutembelea mbuga za wanyama za Serengeti na Ngorongoro na kusema kwamba ni maeneo mazuri ambayo hajawahi kuyaona tangu azaliwe.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMATANO, SEPTEMBA 13, 2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na Balozi wa Iran. Mousa Farhang nakufanya mazungumzo ya kikazi leo Septemba 13/2017.Ofisini kwake Magogoni Dar es salaam. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


Hivyo makala TANZANIA IPO SALAMA NA IMARA -WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

yaani makala yote TANZANIA IPO SALAMA NA IMARA -WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA IPO SALAMA NA IMARA -WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/tanzania-ipo-salama-na-imara-waziri.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TANZANIA IPO SALAMA NA IMARA -WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA"

Post a Comment

Loading...