Loading...
title : Ujamaa na Polisi zatinga nusu fainali kombe la mtoano
link : Ujamaa na Polisi zatinga nusu fainali kombe la mtoano
Ujamaa na Polisi zatinga nusu fainali kombe la mtoano
Kikosi cha Timu ya Polisi
Kikosi cha timu ya Ujamaa
Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Timu za Ujamaa na Polisi zimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali kwenye Kombe la Mtoano linaloendelea kwenye Dimba la Amaan.
Polisi wamewatoa El Hilal kwa penalti 5-4 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 kwenye dakika ya 90 ya mchezo huo uliopigwa saa 10 za jioni jana.
Bao la Polisi limefungwa na Mohd Hassan dakika ya 16 huku bao la El Hilal wakisawazisha dakika ya 86 kupitia Juma Makame.
Na wakati wa saa 8 za mchana Ujamaa Sports Club wakaitoa Raskazone kwa kuifunga bao 1-0 kwenye mchezo huo.
Kwa matokeo hayo Polisi na Ujamaa wataungana na Shaba pamoja na Hawai kucheza hatua ya nusu fainali kwenye mashindano hayo ambapo bado haijajulikana lini na nani atacheza na nani.
Mashindano hayo yameandaliwa na Chama cha Soka cha Wilaya ya Mjini ambapo yalishirikisha vilabu 16 kwa madaraja tofauti vikiwemo vya ligi kuu soka ya Zanzibar, Daraja la Kwanza Taifa, Daraja la Pili Taifa, Daraja la Pili Wilaya na Daraja la Tatu .
Hivyo makala Ujamaa na Polisi zatinga nusu fainali kombe la mtoano
yaani makala yote Ujamaa na Polisi zatinga nusu fainali kombe la mtoano Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Ujamaa na Polisi zatinga nusu fainali kombe la mtoano mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/ujamaa-na-polisi-zatinga-nusu-fainali.html
0 Response to "Ujamaa na Polisi zatinga nusu fainali kombe la mtoano"
Post a Comment