Loading...
title : DC SHINYANGA AFUNGA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA 'MGAMBO' WILAYA YA SHINYANGA
link : DC SHINYANGA AFUNGA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA 'MGAMBO' WILAYA YA SHINYANGA
DC SHINYANGA AFUNGA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA 'MGAMBO' WILAYA YA SHINYANGA
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefunga mafunzo ya Jeshi la Akiba “Mgambo” wilaya ya Shinyanga ambapo jumla ya wahitimu 238 wamefuzu mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa miezi minne.
Sherehe za kufunga mafunzo hayo zimefanyika leo Jumatatu Oktoba 9,2017 katika viwanja vya Sabasaba mjini Shinyanga.Akizungumza katika sherehe hizo,Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kutumia vyema mafunzo waliyoyapata huku akiwaasa kufanya shughuli za maendeleo ili kujiinua kiuchumi.
Matiro aliwataka wahitimu hao kuunda vikundi vya ujasiriamali ili serikali iweze kuwasaidia. “Mmejifunza mambo mengi,naomba muzingatie mlichojifunza,muwe wazalendo wa nchi yetu,kuweni mstari wa mbele kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa kuwafichua wahalifu na wale wote wanaoleta uvunjifu wa amani katika jamii”,aliongeza Matiro.
Katika hatua nyingine alizitaka kampuni za ulinzi kutumia walinzi waliopitia mafunzo ya mgambo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikagua gwaride
Wahitimu wa mafunzo hayo wakisubiri kukaguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Wahitimu wa mafunzo hayo wakisubiri kukaguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Wahitimu wa mafunzo hayo wakisubiri kukaguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Hivyo makala DC SHINYANGA AFUNGA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA 'MGAMBO' WILAYA YA SHINYANGA
yaani makala yote DC SHINYANGA AFUNGA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA 'MGAMBO' WILAYA YA SHINYANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC SHINYANGA AFUNGA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA 'MGAMBO' WILAYA YA SHINYANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/dc-shinyanga-afunga-mafunzo-ya-jeshi-la.html
0 Response to "DC SHINYANGA AFUNGA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA 'MGAMBO' WILAYA YA SHINYANGA"
Post a Comment