Loading...
title : NAIBU WAZIRI SHONZA AHIDI KUSIMAMIA MAADILI YA MTANZANIA
link : NAIBU WAZIRI SHONZA AHIDI KUSIMAMIA MAADILI YA MTANZANIA
NAIBU WAZIRI SHONZA AHIDI KUSIMAMIA MAADILI YA MTANZANIA
Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ameahidi kushirikiana na Watendaji wa Wizara, wadau pamoja na wananchi kwa ujumla kusimamia maadili ya Mtanzania ili kuendelea kuwa na taifa bora.
Mhe. Shonza ameyasema hayo alipowasili katika ofisi za Wizara leo mjini Dodoma ambapo alipokelewa na Waziri mwenye dhamana Dkt. Harrison Mwakyembe, viongozi wa Wizara pamoja na watumishi.
“Wizara hii ni muhimu sana kwa kuwa inajenga taswira ya taifa kupitia sekta zake ambazo ni Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo hivyo ntahakikisha tunashirikiana kwa karibu katika kuwatumikia wananchi “alisema Naibu Waziri Shonza.
Aliongeza kwa kueleza kuwa atahakikisha suala la maadili bora kwa jamii linazingatiwa ili kuendelea kujenga taifa imara kwa kuzingatia mavazi yenye heshima na nyimbo zenye kujenga.
Aidha, Naibu Waziri Shonza amesema ni wajibu wetu kama watumishi wa umma kuhakikisha tunatekeleza Ilani ya chama tawala ambacho kiliahidi kuwatumikia watanzania ili kuhakikisha malengo ya Serikali yanafikiwa kwa wakati.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akikabidhiwa ofisi na aliyekuwa Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura leo mjini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) baada ya kuwasili ofisini leo mjini Dodoma. Wa kwanza kulia ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizra hiyo Mhe. Anastazia Wambura.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na baadhi ya viongozi na watumishi wa Wizara wakati wa kumkaribisha Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Nuru Millao.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (wa pili kushoto) akiongea na baadhi ya viongozi wa Wizara akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kushoto) mara baada ya kuwasili ofisini mjini Dodoma. Wa kwanza kulia ni aliyekuwa Naibu Waziri wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala NAIBU WAZIRI SHONZA AHIDI KUSIMAMIA MAADILI YA MTANZANIA
yaani makala yote NAIBU WAZIRI SHONZA AHIDI KUSIMAMIA MAADILI YA MTANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI SHONZA AHIDI KUSIMAMIA MAADILI YA MTANZANIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/naibu-waziri-shonza-ahidi-kusimamia.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI SHONZA AHIDI KUSIMAMIA MAADILI YA MTANZANIA"
Post a Comment