Loading...
title : WALIOKUWA MAOFISA WA TANTRADE WAHUKUMIWA MIAKA 3 JELA AU FAINI YA MILIONI 20.
link : WALIOKUWA MAOFISA WA TANTRADE WAHUKUMIWA MIAKA 3 JELA AU FAINI YA MILIONI 20.
WALIOKUWA MAOFISA WA TANTRADE WAHUKUMIWA MIAKA 3 JELA AU FAINI YA MILIONI 20.
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.
MKURUGENZI wa Utafiti na Mipango wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Samweli Mvingira na Naibu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Judith Msuya, wamehukumiwa kwenda jela miaka mitatu ama kulipa faini ya Milioni 20 baada ya kupatikana na hatia katika kosa la kutumia madaraka vibaya.
Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha ambaye amesema upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka dhidi washtakiwa pasipo kuacha shaka.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkeha amesema amewatia hatiani washtakiwa kwa makosa manne ya kutumia madaraka yao vibaya na kuwaachia huru katika kosa la tano ambalo jamuhuri wameshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.
Katika kesi hiyo washtakiwa walikuwa watatu akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade ambaye alifariki wakati shahidi wa kwanza akitoa ushahidi.
Inadaiwa, kati ya September 2007 na July 2008, Makao Makuu ya TanTrade Wilaya ya Temeke walitumia madaraka yao vibaya kwa kuagiza gari lililotumika kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma iliyosababisha AL Hamadi Motors FZD kupata faida ya Tsh. 34,895,400.
Aidha, inadaiwa tarehe hiyo hiyo na mahali hapo, washtakiwa kwa kutumia madaraka yao vibaya, walinunua gari iliyotumika kwa lengo la kumnufaisha Humer Stars kiasi cha Tsh. 32,773,475.
Washtakiwa wanadaiwa bila kufuata utaratibu wa kushindanisha zabuni kuagiza gari iliyotumika na kusababisha AL Hamad kupata faida ya Tsh. 34,895,400, hata hivyo katika shtaka la nne watuhumiwa walinunua magari bila kufuata utaratibu wa zabuni.
Pia washtakiwa waliachiwa huru ambapo Jamuhuri ilishindwa kuthibitisha, washtakiwa walidaiwa kutumia madaraka yao vibaya, uzembe na kumsababishia mwajiri wao hasara ya Tsh. 49,145,855.05.
Hata hivyo, mshtakiwa Mvingira amefanikiwa kulipa faini na yuko huru.
Hivyo makala WALIOKUWA MAOFISA WA TANTRADE WAHUKUMIWA MIAKA 3 JELA AU FAINI YA MILIONI 20.
yaani makala yote WALIOKUWA MAOFISA WA TANTRADE WAHUKUMIWA MIAKA 3 JELA AU FAINI YA MILIONI 20. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WALIOKUWA MAOFISA WA TANTRADE WAHUKUMIWA MIAKA 3 JELA AU FAINI YA MILIONI 20. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/waliokuwa-maofisa-wa-tantrade.html
0 Response to "WALIOKUWA MAOFISA WA TANTRADE WAHUKUMIWA MIAKA 3 JELA AU FAINI YA MILIONI 20."
Post a Comment