Loading...

Maandalizi ya Utafiti wa mafuta Ziwa Eyasi, Tanganyika Yaanza

Loading...
Maandalizi ya Utafiti wa mafuta Ziwa Eyasi, Tanganyika Yaanza - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Maandalizi ya Utafiti wa mafuta Ziwa Eyasi, Tanganyika Yaanza, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Maandalizi ya Utafiti wa mafuta Ziwa Eyasi, Tanganyika Yaanza
link : Maandalizi ya Utafiti wa mafuta Ziwa Eyasi, Tanganyika Yaanza

soma pia


Maandalizi ya Utafiti wa mafuta Ziwa Eyasi, Tanganyika Yaanza



Asteria Muhozya na Greyson Mwase. 

Timu ya wataalam kutoka Uganda imewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na wataalam wa Tanzania katika utafiti wa mafuta. Mbali na kubadilishana uzoefu wataalam hao watafanya ziara Ziwa Eyasi Wembere lililopo mkoani Singida.

Kabla ya kuanza kwa ziara hiyo wataalam hao leo tarehe 2 Oktoba, 2017 wamefanya kikao kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani na kuwashirikisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo pamoja na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA).

Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Kalemani amesema maandalizi hayo ni juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli za kuhakikisha kuwa rasilimali ya mafuta inagunduliwa na kuanza kuleta manufaa kwa wananchi, ambapo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la Ujenzi wa Mradi ya Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania tarehe 5 Agosti, 2017 alieleza kuwa wataalam waliogundua mafuta katika Ziwa Abert nchini Uganda kushirikiana na wataalam wa Tanzania katika utafiti wa mafuta katika Ziwa Tanganyika na Eyasi nchini Tanzania.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha wataalam kutoka Uganda, Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ua Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) kabla ya kuanza ziara katika Ziwa Eyas Wembere lililopo mkoani Singida. 
Wataalam kutoka , Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ua Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani). 
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Robert Kasande (kulia) pamoja na wataalam kutoka Uganda wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto mbele) akieleza jambo katika kikao hicho.



Hivyo makala Maandalizi ya Utafiti wa mafuta Ziwa Eyasi, Tanganyika Yaanza

yaani makala yote Maandalizi ya Utafiti wa mafuta Ziwa Eyasi, Tanganyika Yaanza Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Maandalizi ya Utafiti wa mafuta Ziwa Eyasi, Tanganyika Yaanza mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/maandalizi-ya-utafiti-wa-mafuta-ziwa_2.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Maandalizi ya Utafiti wa mafuta Ziwa Eyasi, Tanganyika Yaanza"

Post a Comment

Loading...