Loading...
title : TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA
link : TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA
TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaongeza jitihada za kuzuia na kupunguza ajali za barabarani kwa kuhakikisha madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatii sheria za usalama barabarani. Aidha kumekuwa na ajali 01 ya kifo kama ifuatavyo:-
Mnamo tarehe 26.11.2017 majira ya saa 10:00 Asubuhi huko Maeneo ya Kadege, Kata ya Forest, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya, Gari yenye namba za usajili T.913 BEW aina ya Toyota Ipsum iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aitwaye MUGANIZI RAPHAEL [34] Mkazi wa Simike iligongana na gari yenye namba za usajili T.204 CSZ/T.670 BEZ aina ya Scania Lory ikiendeshwa na HOSEA S/O MWASHAMBWA [28] Mkazi wa Uyole na kusababisha kifo kwa dereva wa Gari yenye namba za usajili T.913 BEW Toyota Ipsum.
Chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa gari yenye namba za usajili T.913 BEW Toyota Ipsum hasa ukizingatia eneo hilo ni lenye mteremko mkali. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya. Dereva wa lori alikimbia mara baada ya ajali na juhudi za kumtafuta zinaendelea. Upelelezi unaendelea.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na matukio makubwa ya uhalifu pamoja na wahalifu. Jitihada zinaendelea kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha Mkoa wetu unakuwa mahala salama. Hata hivyo Kumekuwa na matukio 02 ya mauaji kama ifuatavyo:-
Mnamo tarehe 25.11.2017 majira ya saa 22:06 usiku huko katika Kijiji cha Ipwizi, Kata ya Mjele, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la MINZA PAUL [25] Mkazi wa Ipwizi alifariki dunia baada ya kupigwa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na mume wake aliyefahamika kwa jina SHILONDI MAKWENGE ambaye alitoroka baada ya tukio.
Hivyo makala TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA
yaani makala yote TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/taarifa-kutoka-jeshi-la-polisi-mkoani.html
0 Response to "TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA"
Post a Comment