Loading...
title : BURIANI ALHAJ SHEIKH AHMED ISLAM
link : BURIANI ALHAJ SHEIKH AHMED ISLAM
BURIANI ALHAJ SHEIKH AHMED ISLAM
Na Ramadhani K. Dau, Malaysia
Ilikuwa siku ya Jumamosi tarehe 23 Disemba 2017, majira ya saa 5 usiku kwa saa za Malaysia nilipopata ujumbe mfupi wa sms kutoka kwa Sheikh Issa Othman, maarufu Mufti wa London, Imam wa Masjid Maamur ukiniarifu msiba wa mzee wetu Sheikh Ahmed Islam. Ujumbe wake ulikuwa mfupi sana: “Mzee wetu Ahmed Islam amefariki sasa hivi. Maiti inaletwa msikitini hivi sasa. Maziko kesho In Shaa Allah. Innallillahi Wainnaillahi Raajiuun”.
Mara tu baada ya kupata taarifa hiyo na baada ya kumtakia maghfira mzee wetu, nikajua kuwa kwa mara nyingine tena umeniangukia wajibu wa kuandika Taazia ya mtu ambaye namfahamu, namheshimu na alikuwa na ukaribu sana na mimi. Nimeshawahi kuandika huko nyuma kuwa kuandika Taazia ni jambo zito na gumu sana. Kila niandikapo hutamani sana Taazia hiyo iwe ndio ya mwisho.
Lakini kwa mipango Yake Mwenyezi Mungu, najikuta nashindwa kukwepa wajibu huo. Hata hivyo, mara hii nilidhani ningeweza kuukwepa wajibu huo kwa kumuomba rafiki yangu na ndugu yangu mwanahistoria maarufu Sheikh Mohamed Said aandike Taazia hiyo nami nilikuwa tayari kumpa maelezo yoyote ambayo yangemsaidia katika uandishi wake. Pamoja ya kuwa alikubali kuifanya kazi hiyo, Mohamed alisisitiza kuwa lazima na mimi niandike. Kwa jinsi ya msisitizo aliouweka Sheikh Mohamed, nimejikuta kwa mara nyingine tena nalazimika kuandika Taazia hii huku nikiwa na moyo wa huzuni sana kwa kuondokewa na mzee wangu ambaye alikuwa mithili ya baba yangu mzazi.

Marehemu mzee Ahmed Islam ana mambo mengi na sura nyingi. Wapo wanaomfahamu kama ni miongoni mwa wazee maarufu na viongozi katika jamii ya Waislamu, wapo wanaomfahamu kama mtaalamu wa masuala ya Rasilimali Watu (Human Resources) na wapo wanaomfahamu mzee Ahmed Islam kama mwana michezo mahiri.
Marehemu mzee Ahmed Ijhad Islam alizaliwa Zanzibar tarehe 22 Disemba 1930 akiwa ni mtoto pekee wa Sheikh Ijhad Islam na bibi yetu Bi Maryam Mussa. Kwa bahati mbaya, mzee Ijhad Islam alifariki wakati mzee Ahmed akiwa mdogo na hivyo akalelewa na mama yake. Baada ya msiba huo, bibi yetu Bi Maryam aliolewa na kupata mtoto mmoja wa kike ambaye jina lake ni Zerah.
Baada ya kumaliza masomo yake ya msingi na Sekondari kwenye Government School (sasa Ben Bella) Zanzibar mwaka 1948, ilipofika mwaka 1957 marehemu mzee Ahmed Islam alikwenda Cornwall, Uingereza kuchukua masomo katika fani ya Mawasiliano yaani Telecommunications. Wakati huo alikuwa ameajiriwa na kampuni ya Cable and Wireless (C&W) ambako alikuwa Meneja Msaidizi (Assistant Manager). Kampuni hii ilikuwa ndiyo kampuni kubwa ya mawasiliano Afrika Mashariki. Baada ya kurudi masomoni, marehemu aliendelea na kazi yake na baada ya kampuni ya C&W kumezwa na Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki (East African Post and Telecommunication), mzee Islam akahamia Dar es Salaam mwaka 1970.
Akiwa Dar es Salaam mzee Islam alifanyakazi katika Shirika hilo na baada ya mgawanyiko yakaundwa Mashirika mawili tofauti; Shirika la Posta (TPC) na Shirika la Simu (TTCL).
Marehemu mzee Islam alihamishiwa TTCL hadi alipostaafu mwaka 1986 akiwa katika nafasi ya Mkurugenzi wa Rasilimali Watu yaani Director of Manpower. Baada ya kustaafu, marehemu alifanyakazi Ubalozi wa Ufaransa kwa mkataba wa miaka 3. Wakati wa uhai wake, mzee Islam amefanya mengi katika fani mbalimbali ikiwa ni pamoja na uongozi wa dini, ujenzi wa nchi, uendelezaji wa michezo na utoaji nasaha kwa Taasisi na vijana mbalimbali katika masuala ya ndoa na kujiendeleza kwenye elimu ya juu.

Kwa upande wa dini, marehemu ametoa mchango mkubwa sana. Miongoni mwa matunda ya kazi yake ni usimamizi wa ujenzi wa Masjid Maamur iliyopo Upanga, Dar es Salaam.
Kwa wanaokumbuka vizuri jiografia ya Upanga, kabla 1987 pale palipojengwa Masjid Maamur hapakuwa na msikiti. Lakini kwa kushirikiana na wazee wenziwe marehemu mzee Islam aliweza kusimama kidete katika kusimamia ujenzi wa Masjid. Si wengi wanaofahamu kuwa ujenzi wa Masjid Maamur ulianza na msukusuko mkubwa kwa sababu kulikuwa na mwanajeshi ambaye alikuwa amepanga kwenye nyumba ya jirani ambayo ilikuwa inamilikiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Hivyo makala BURIANI ALHAJ SHEIKH AHMED ISLAM
yaani makala yote BURIANI ALHAJ SHEIKH AHMED ISLAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BURIANI ALHAJ SHEIKH AHMED ISLAM mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/buriani-alhaj-sheikh-ahmed-islam.html
0 Response to "BURIANI ALHAJ SHEIKH AHMED ISLAM"
Post a Comment