Loading...
title : JARADA KESI YA AVEVA, KABURU LARUDISHWA TAKUKURU
link : JARADA KESI YA AVEVA, KABURU LARUDISHWA TAKUKURU
JARADA KESI YA AVEVA, KABURU LARUDISHWA TAKUKURU
Baada ya malalamiko ya muda mrefu, hatimae mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amerejesha TAKUKURU Jalada la uchunguzi la kesi ya utakatishaji wa USD 300,000, inayowakabili Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake,Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu na kuelekeza uchunguzi zaidi ufanyike.
Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai ameewleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa kesi hiyo ilipokuja kutajwa,
Pia alidai kuwa jalada la kesi hiyo lililokuwepo kwa DPP limekwisha rejeshwa na ameelekeza uchunguzi zaidi ufanyike na kwamba uchunguzi huo umekwishaanza kuwa ajili ya kukamilisha maeneo ambayo DPP ameelekeza.
Aidha amedai wanaomba ufunguo kutoka kwa mshtakiwa Aveva ili waweze kupata nyaraka ikiwa sehemu ya kukamilisha upelelezi.
Amedai Aveva alikuwa na ofisi mbili, ya Simba na binafsi na kwamba katika ofisi hiyo binafsi kuna nyaraka za Simba na kuwa walimuandikia barua kupitia gerezani ili aweze kuruhusu upatikanaji wa funguo ili wapate nyaraka zinazohitajika lakini hawajajibiwa. Swai aliomba upande wa utetezi uharakishe wapate hizo nyaraka ili waweze kukamilisha upelelezi.
Wakili wa utetezi, Evodius Mtawala aliieleza mahakama kuwa Aveva ameipata barua hiyo na kwamba juhudi zinaendelea kufanyika na nyaraka zilizoombwa zinaendelea kukusanywa na zitawasilishwa hivi karibuni.
Baada ya kutolewa maelezo hayo, Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hadi Desemba 28, mwaka huu.
Katika kesi hiyo, Evans Aveva na makamu wake, Kaburu wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha USD 300,000.
Hivyo makala JARADA KESI YA AVEVA, KABURU LARUDISHWA TAKUKURU
yaani makala yote JARADA KESI YA AVEVA, KABURU LARUDISHWA TAKUKURU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JARADA KESI YA AVEVA, KABURU LARUDISHWA TAKUKURU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/jarada-kesi-ya-aveva-kaburu-larudishwa.html
0 Response to "JARADA KESI YA AVEVA, KABURU LARUDISHWA TAKUKURU"
Post a Comment