Loading...

Madabida na wenzake wapelekwa rumande hadi Decemba 15

Loading...
Madabida na wenzake wapelekwa rumande hadi Decemba 15 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Madabida na wenzake wapelekwa rumande hadi Decemba 15, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Madabida na wenzake wapelekwa rumande hadi Decemba 15
link : Madabida na wenzake wapelekwa rumande hadi Decemba 15

soma pia


Madabida na wenzake wapelekwa rumande hadi Decemba 15

Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imetupilia mbali hoja za mawakili  wa utetezi na kuuamuru upande wa jamhuri kuhakikisha tarehe ya kutajwa kwa shauri hilo wawe wameshawasilisha taarifa za kesi Mahakama Kuu ya Uhujumu Uchumi au wawasilishe kibali cha DPP kuipa mamlaka mahakama ya Kisutu kusikiliza kesi hiyo ili taratibu za dhamana zifanyike.

Kufuatia uamuzi huo aliyekuwa mwenyekiti wa  CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na wenzake watano wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, wamepelekwa gerezani kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Uamuzi huo uliotolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Victoria Nongwa umetokana na hoja zilizowasilishwa juzi na mawakili wa utetezi wakiongozwa na Dennis Msafiri kwamba mahakama hiyo  ina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi ambalo linahusisha shilingi milioni 148.

Hata hivyo, mawakili wa serikali Pius Hilla na Shadrack Kimaro walipinga hoja hiyo na kudai mahakama haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo kwa kuwa linasikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi na DPP haijaipa kibali cha kuisikiliza.
Hakimu Victoria alisema shitaka la sita linalowakabili washtakiwa ni la uhujumu uchumi na tatizo lililoko ni wakati gani DPP anaweza kuwasilisha kibali cha kuipa mamlaka mahakama.
Alisema katika hilo sheria ipo kimya na kwamba washitakiwa hao walifikishwa mahakamani 2014  na kesi ilikuwa na kibali cha DPP na wameweza kuhudhuria kesi hadi Desemba 6, mwaka huu, ambapo DPP aliamua kuiondoa kesi ikiwa tayari mashahidi saba wa upande wa jamhuri wameshatoa ushahidi wao huku watatu wakiwemo mahakamani hapo kwa ajili ya kutoa ushahidi.
Hakimu Nongwa amesema siku hiyo, washitakiwa hao walifunguliwa kesi ya uhujumu uchumi hivyo kama kweli upande wa jamhuri una nia ya kutenda haki na haki ionekane imetendeka ni vema shauri hilo lianze kusikilizwa.
"Tunapokuja tarehe nyingine muwe mmefaili taarifa Mahakama Kuu ya Uhujumu Uchumi au mlete kibali cha DPP au muondoe mashtaka" alisisitiza Hakimu Nongwa.
Hakimu Victoria alitupilia mbali hoja za upande wa utetezi na kusema wanasubiri kibali cha DPP ili taratibu za dhamana ziendelee au wawasilishe taarifa Mahakama Kuu.
Kesi hiyo itatajwa tena, Desemba 15, mwaka huu, washtakiwa wamepelekwa mahabusu.
Madabida na wenzake waliposomewa mashitaka Desemba 6, mwaka huu , mbele ya Hakimu Victoria, muda mfupi baada ya kufutiwa kesi ya awali hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa kesi hiyo ni ya uhujumu uchumi.
Washtakiwa wote wanakabiliwa na mashitaka sita ya kula njama,  kusambaza dawa bandia za kufubaza virusi vya ukimwi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuisababishia MSD hasara ya milioni 148.
Mbali na Madabida wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Seif Shamte ambaye ni mkurugenzi  wa uendeshaji,  Simon Msoffe (meneja masoko) na  Fatma Shango (mhasibu msaidizi) wa Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd.

Pia wamo ni Sadick Materu na Evans Mwemezi ambao ni maofisa wa Bohari Kuu ya Dawa. 


Hivyo makala Madabida na wenzake wapelekwa rumande hadi Decemba 15

yaani makala yote Madabida na wenzake wapelekwa rumande hadi Decemba 15 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Madabida na wenzake wapelekwa rumande hadi Decemba 15 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/madabida-na-wenzake-wapelekwa-rumande.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Madabida na wenzake wapelekwa rumande hadi Decemba 15"

Post a Comment

Loading...