Loading...

MBUNGE AZZA HILAL AKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 6.8 KUKAMILISHA UJENZI WA WODI YA WAZAZI ZAHANATI YA SOLWA

Loading...
MBUNGE AZZA HILAL AKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 6.8 KUKAMILISHA UJENZI WA WODI YA WAZAZI ZAHANATI YA SOLWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MBUNGE AZZA HILAL AKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 6.8 KUKAMILISHA UJENZI WA WODI YA WAZAZI ZAHANATI YA SOLWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MBUNGE AZZA HILAL AKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 6.8 KUKAMILISHA UJENZI WA WODI YA WAZAZI ZAHANATI YA SOLWA
link : MBUNGE AZZA HILAL AKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 6.8 KUKAMILISHA UJENZI WA WODI YA WAZAZI ZAHANATI YA SOLWA

soma pia


MBUNGE AZZA HILAL AKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 6.8 KUKAMILISHA UJENZI WA WODI YA WAZAZI ZAHANATI YA SOLWA

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad (CCM) (wa pili kushoto) amekabidhi hundi ya shilingi Milioni 6.8 ( 6,830,000/=) kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi katika zahanati ya kijiji cha Solwa kilichopo kata ya Solwa jimbo la Solwa mkoani Shinyanga. mAkizungumza Jumamosi Desemba 30,2017 wakati wa kukabidhi hundi hiyo kwa kamati ya ujenzi wa zahanati hiyo, alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi aliyotoa alipotembelea zanahati hiyo mwezi Mei mwaka huu na kukuta changamoto ya uhaba wa vyumba vya kutolea huduma za afya ikiwemo wodi ya watoto na akina mama. 

“Nilifanya ziara katika zanahati hii mwezi Mei mwaka huu wakati natoa vitanda vya kujifungulia na viti vya wagonjwa,baada ya kuingia katika chumba cha akina mama nilikuta vitanda vitatu,niliguswa na jinsi akina mama walivyokuwa wanahangaika,lakini nikaambiwa wananchi wana mpango wa kujenga wodi ya watoto na akina mama,nikaahidi kuchangia mabati 20 pindi majengo yatakapofikia hatua ya upauaji”,alieleza mbunge huyo. 

“Mwezi Septemba mwaka huu, Diwani wa kata ya Solwa alinitumia picha za majengo mawili yakiwa tayari kwa upauaji, nikawaza kuhusu mabati yangu 20, nikaona hayatoshi, ndipo nikaamua kuanza kutafuta watu wa kunisaidia, juzi nikapokea ujumbe kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF kuwa wamekubali ombi langu na wameamua kutoa shilingi 6,830,000/= kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo moja”, alieleza. 

Alisema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kununua mabati na mbao pamoja shughuli zingine katika kukamilisha ujenzi wa jengo la wodi ya akina mama katika zahanati ya Solwa iliyojengwa kwa michango ya wananchi wa kijiji cha Solwa. 

“Niwapongeze sana watu wa Solwa kwa kuamua kuchangishana na kuanza ujenzi, Solwa itajengwa na Wana Solwa,hili ni jibu tosha kabisa kwamba kila kilio kina mwenyewe,mlichokifanya kinapaswa kuigwa katika maeneo mengine,niwashukuru sana pia NSSF kwa kunishika mkono ili kuokoa maisha ya akina mama na watoto”,aliongeza Azza Hilal Hamad. 

Hata hivyo aliwataka wananchi wa Solwa kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili iwe na manufaa kwa wananchi. 

Mbunge huyo alitumia fursa hiyo pia kuwakumbusha wazazi na walezi kupeleka watoto shule badala ya kuwaozesha wangali wadogo kwa tamaa ya mali huku akisisitiza kuwa urithi mzuri kwa mtoto ni elimu pekee. 

“Ni marufuku kuozesha watoto wa kike wanafunzi,matokeo ya darasa saba yametoka,wote waliofaulu wapelekwe shule,waliofeli nao watafutieni kazi zingine za kufanya siyo kuwaozesha,kufeli shule siyo kufeli maisha”,aliongeza. 

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kijiji Solwa, George Bushiya alisema baada ya wananchi kukerwa na adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya walikubaliana kuchangishana fedha ili kujenga majengo ya wodi ya watoto na akina mama ambapo zaidi ya shilingi milioni 36 zimetumika mpaka sasa. 

Kaimu Mganga Mkuu wa halmashauri ya Shinyanga, Dk. Salim Matondo alimshukuru mbunge huyo kwa kusaidia ujenzi wa wodi ya akina mama ambapo pindi ujenzi utakapokamilika itasaidia kupunguza adha ya akina mama kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya katika hospitali ya Nindo na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga. 
Muonekano wa majengo mawili yaliyojengwa na wananchi wa kijiji cha Solwa yatakayotumika kama wodi ya watoto na akina mama katika zahanati ya Solwa iliyopo katika kijiji cha Solwa,kata ya Solwa,jimbo la Solwa mkoani Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati wa kukabidhi hundi ya shilingi Milioni 6.8 ( 6,830,000/=) kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi katika zahanati ya kijiji cha Solwa kilichopo kata ya Solwa jimbo la Solwa mkoani Shinyanga. 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akimsalimia mama aliyejifungua mtoto wa kike mara baada tu ya mbunge kufika katika zanahati hiyo.Mama huyo alikuwa amepewa rufaa ya kwenda kujifungulia katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga,lakini kutokana na Kaimu Mganga Mkuu wa halmashauri ya Shinyanga,Dk. Salim Matondo kuhudhurika kikao cha mbunge,ndiyo ikawa fursa nzuri kwa mama huyo kupewa huduma na Daktari huyo 
Mbunge Azza Hilal Hamad akiwa amembeba mtoto aliyepewa jina la "Azza" 
Mbunge Azza Hilal Hamad akifurahia jambo baada ya kumpatia zawadi ya vitenge mama aliyejifungua mtoto wa kike katika zahanati ya Solwa. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.


Hivyo makala MBUNGE AZZA HILAL AKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 6.8 KUKAMILISHA UJENZI WA WODI YA WAZAZI ZAHANATI YA SOLWA

yaani makala yote MBUNGE AZZA HILAL AKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 6.8 KUKAMILISHA UJENZI WA WODI YA WAZAZI ZAHANATI YA SOLWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MBUNGE AZZA HILAL AKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 6.8 KUKAMILISHA UJENZI WA WODI YA WAZAZI ZAHANATI YA SOLWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/mbunge-azza-hilal-akabidhi-hundi-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MBUNGE AZZA HILAL AKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 6.8 KUKAMILISHA UJENZI WA WODI YA WAZAZI ZAHANATI YA SOLWA"

Post a Comment

Loading...